Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Makampuni ya Bima nchini
(ATI), Khamis Suleiman akizungumza katika hafla hiyo ya kuaga mwaka
2019 na kuukaribisha mwaka 2020, hafla iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wamiliki mbalimbali wa Makampuni ya Bima wakifurahi katika hafla hiyo
yakuaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2020, hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko kutoka Mamlaka ya
Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) Samwel Mwiru akizungumza katika hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Taasisi za Bima zimetakiwa kufika mikoa mbalimbali ambayo haijafikiwa na huduma za Bima ili kuhakikisha inaondokana na uhaba wa huduma hizo kila sehemu kwa kutoa fursa zaidi kwa wakulima na watu wenye kipato cha chini.
Wito huo umetolewa leo Desemba 18, 2019 na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Makampuni ya Bima nchini (ATI), Khamis Suleiman wakati wa hafla ya kuaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka 2020, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Khamis amesema mwaka 2020, Taasisi hiyo na Mamlaka husika imetenga bajeti kubwa kuhamasisha Wananchi kupata elimu ya Bima, amesema pia Taasisi hizo zinapaswa kufika mikoa ambayo ina uhaba wa huduma za Bima ili kuwa na uwiano sawa na mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.
Amesema kazi kubwa ya Chama cha Wamiliki Bima kinahakikisha huduma za Bima zinawafikia Wananchi kwa bei nafuu, pamoja na kutoa mchango mkubwa kwenye Uchumi wa nchi ambao kwa sasa ni 1% ya pato la Taifa na lengo ni kutoa 3% katika miaka mitatu ijayo.
Amesema Chama hicho kimepata mafanikio katika mwaka 2019 kwenye kusimamia bei sahihi za Bima hizo kwa wananchi, kuzuia hasara kwa Kampuni hizo, kuchangia Kodi Sirikalini.
"Mwaka 2018 kulikuwa na changamoto nyingi sana nafikiri mahesabu yatakuwa mazuri zaidi mwaka 2019, lakini changamoto bado zipo tunajitahidi kuzitatua changamoto hizo, na changamoto kubwa ni Elimu ya Bima kwa wananchi hawaelewi kuhusu faida za Bima, mwaka 2020 kutakuwa na mafanikio zaidi kuliko 2019," amesema Khamis Suleiman.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) Samwel Mwiru amesema wananchi wamezidi kuwa na hamasa katika huduma za Bima mwaka hadi mwaka licha yaku na uboreshaji kwenye hamasa hiyo.
Mwiru ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa kukata Bima kwa manufaa yao, amesema Watanzania wanakila sababu yakuchangamkia fursa hiyo kutokana na uwepo wa Kampuni 32 za utoaji huduma za Bima, Madalali wanaotoa huduma hizo 130, Mawakala zaidi ya 600 kote nchini.
Amesema changamoto kubwa katika Sekta ya Bima, Wananchi wengi hawana elimu kuhusu Bima, amesema Mamlaka hiyo (TIRA) na Makampuni yanawajibu kuelimisha wananchi hao kuhusu umuhimu huduma hizo na kuwafikishia kwa njia mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...