Waogeleaji chipukizi wakichumpa
wakati wa mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kisasa la Shule ya
Kimataifa ya Tanganyika (IST)- Masaki.

Waogeleaji chipukizi wakiwa katika pozi baada ya kuzawadiwa medali zao kwa kushinda ‘relay’

Mama na Mwana! Meneja wa timu ya
Taliss-IST, Hadija Shebe akisheherekea na mwanaye, Nawal Shebe wakati wa
mashindano ya kuogelea ya yoso chini ya miaka 12.

Waogeleaji chipukizi wakiwa katikan pozi baada ya kuzwadiwa medali zao.
……………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Klabu ya kuogelea ya Taliss-IST imefanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa kwa waogeleaji wenye umri chini ya miaka 12.
klabu hiyo
imezipiku klabu tisa baada ya kupata jumla ya pointi 1,736 katika
mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la kisasa la Shule ya
Kimataifa ya Tanganyika (IST)- Masaki.
Waogeleaji
wavulana wa klabu hiyo wamechangia pointi nyingi kwa timu yao baada ya
kukusanya 948 huku upande wa wanawake wakipata pointi 788.
Meneja wa
Taliss-IST, Hadija Shebe aliwapongeza wachezaji wake kwa kuendeleza
ushindi katika mchezo huo na kuiletea sifa klabu yao.
“Siri kubwa ya
ushindi kwa klabu yetu ni ushirikiano baina ya wazazi, makocha na moyo
wa kujituma kwa waogeleaji, nawapongeza wachezaji kwa kufanya vyema,”
alisema Hadija.
Klabu
inayokuja kwa kasi ya Bluefins imemaliza nafasi ya pili kwa kukusanya
pointi 1,521 ambapo kwa upande wa wanawake, klabu hiyo imekuwa ya kwanza
kwa kupata pointi 798 na pointi 723 zilikusanywa na waogeleaji wanaume.
Nafasi ya tatu
imechukuliwa na klabu ya Dar Swim Club (DSC) kwa kupata pointi 779
ambapo kwa upande wa wanawake klabu hiyo ilikusanya pointi 385 na
wanaume walikusanya pointi 394.
Klabu mpya kabisa
katika mchezo huo, FK Blue Marlins imeshika nafasi ya nne kwa kupata
pointi 778 ambapo kwa upande wa wanawake, klabu hiyo ilipata jumla ya
pointi 597 na wanaume pointi 181.
Nafasi ya tano
ilichukuliwa na klabu ya Uwcea ya Moshi kwa kupata pointi 294 huku
Champion Rise ikishika nafasi ya sita kwa pointi 220, Mis Pirahnas ya
Morogoro (150 pointi, nafasi ya saba), Wahoo Zanzibar (106 pointi,
nafasi ya nane), Mwanza (98 pointi, nafasi ya tisa na nafasi ya 10
ilishikwa na klabu ya Arusha iliyopata pointi tano.
Mashindano hayo
yalishirikisha jumla ya waogeleaji zaidi ya 150 ambao walishindana
katika staili mbalimbali ambazo ni freestyle, butterfly, backstroke,
Breaststroke na Individual Medley (IM).
Waogeleaji hao pia walishinda katika ‘relay’ ambayo ilikuwa ya kusisimua na ushidano mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...