Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kampeni ya kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole iliyofanyika katika viwanja vya Stend ya Zamani mjini Singida akizungumza na wananchi juzi kwenye kampeni hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwenye kampeni hiyo.
Kampeni ikiendelea.
Muonekano wa vibanda vya makampuni ya Simu katika kampeni hiyo.
Na Waandishi wetu, Singida.
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole kwa lengo la kuondoa uhalifu unaofanywa mitandaoni.
Aliyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika kampeni ya kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole iliyofanyika katika viwanja vya Stendi ya Zamani mjini Singida.
Dkt. Nchimbi aliwapongeza wananchi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi ili kusajili laini zao za simu na kueleza umuhimu wa simu na manufaa yake ambapo licha ya umuhimu huo wapo watu wamekuwa wakutumia manufaa hayo Vibaya kwa kufanya uhalifu hivyo ili kudhibiti uhalifu huo serikali ameagiza kila anayemiliki simu asajili laini yake kwa alama za vidole.
"Taifa limeona kuna umuhimu wa simu licha ya kuwa hatarishi katika usalama ndio maana limeamua kuboresha huduma hizi, tuunge mkono juhudi hizi."alisema Dkt Nchimbi.
Hata hivyo aliziagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) kuwafuata wananchi huko waliko ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa kusajili laini zao kwa alama za vidole kabla zoezi hilo halijaisha ambapo linatarajiwa kuhitimishwa Disemba 31 mwaka huu.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda alisema takwimu zinaonyesha takribani watanzania 45 milioni wanamiliki simu lakini mpaka sasa waliosajili laini zao za simu kwa alama za vidole ni watanzania 19 milioni tu, hivyo aliwaomba waendeleze kujitokeza ili wakamilishe zoezi hilo kwani tofauti na hapo hawataruhusiwa kutumia laini ambazo hazijakamilishwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...