TEMESA inapenda kukanusha uvumi unaoenea mitandaoni kupitia video pamoja na picha zikielezea kusimama kwa huduma za vivuko katika kivuko cha Kigongo Busisi mkoani Mwanza kutokana na kuwepo kwa magugu maji. Tukio la magugu maji lilitokea siku ya tarehe 24 Desemba 2019 na magugu maji hayo yaliondolewa.

Shughuli za uvushaji abiria zinaendelea kama kawaida katika kivuko cha Kigongo Busisi. TEMESA inapenda kuwataarifu abiria wote waendelee kutumia huduma za kivuko hicho kwakua kipo salama.

Aidha TEMESA inawakumbusha abiria wote kuzingatia matangazo ya usalama yanayotolewa na mabaharia watumiapo vivuko.
Imetolewa na Kitengo cha Masoko Habari na Uhusiano kwa Umma
 
TEMESA
28/12/2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...