Kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikiwa na ujumbe wenye lengo la kupotosha umma kuhusu kupunguzwa idadi ya mabehewa ya treni zinazofanya safari za reli ya kati kutoka Dar es Salaam - Kigoma na kupelekwa njia ya kaskazini (Dar es salaam - Kilimanjaro).

Taarifa hizo si za kweli, Shirika linawaomba wananchi kupuuza taarifa hizo kwani zina lengo la kupotosha na kuharibu taswira ya Shirika kwa kuwa mabehewa ya abiria yanayotumika yana idadi ileile ni behewa kumi na 14 kwa kuhudumia safari za reli ya kati Dar es Salaam – Kigoma. Umma unapaswa kufahamu kwamba mwezi huu wa kumi na mbili ni kipindi cha likizo na msimu wa sikuku hivyo basi kupelekea ongezeko zaidi la abiria kwa njia ya kati.

Hata hivyo Shirika linaendelea na ukarabati wa miundombinu ya Reli kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP na kusababisha njia hiyo kufungwa siku tatu katika wiki tangu mwezi wa saba 2019 kuanzia Dar es Salaam hadi Isaka umbali wa Kilometa 970, hali iliyopelekea kupunguzwa kwa safari za treni zinazotoa huduma ya usafiri wa abiria kuanzia Daresalaam – Kigoma, kutoka utaratibu wa kutembeza treni mara nne kwa wiki hadi mara tatu, kwa kupeleka ordinary treni mara mbili na deluxe mara moja kwa lengo la kupisha shuguli za mradi zikamilike kwa wakati na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, mradi wa uboreshaji wa reli ya kati ni sehemu ya mikakati ya Shirika katika kuboresha huduma za usafiri wa reli nchini ambapo kukamilika kwa mradi huu mwezi Juni 2020 kutaiwezesha reli ya kati kutembea mwendokasi wa hadi Kilometa 70 kwa saa kutoka 35, hivyo kurahisisha shughuli za usafirishaji na kupungua adha ya usafiri kwa abiria na hivi karibuni wadau wa safari wa njia ya reli ya kati ratiba mpya itatolewa kwa ajili ya kurejesha ratiba ya safari mara nne kwa wiki kwa njia ya kigoma.

Shirika linawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu kwa kujenga miundombinu mipya ya reli ya kisasa na kufufua njia za miundombinu ya reli ambayo imeacha kutumika kwa muda mrefu, TRC Imeanza kufufua kwa kanda ya kaskazini na baadae itaendelea katika maeneo mengine ambako reli zimeacha kutumika ili kuhakikisha wadau wa usafiri wa reli nchini wanapata huduma bora na kila mtanzania ananufaika na fursa na faida zinazopatikana kupitia miundombinu ya reli kwa kuwa TRC inajali na kuthamini wadau wanaotumia huduma za TRC nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...