Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka amewataka Wadau wa Alizeti wa Mkoa wa Singida kupanga mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa Alizeti ili kutosheleza mahitaji makubwa ya viwanda vya kusindika alizeti ambavyo vinashindwa kuzalisha mafuta kwa mwaka mzima kutokana na kukosekana kwa malighafi.
Rutageruka ametoa wito huo wakati akiongea na Wasindikaji, wakulima wa alizeti na watendaji wa Serikali wakati wa Mkutano na Wadau wa alizeti wa Mkoa wa Singida uliofanyika leo tarehe 11.12.2019 katika Ukumbi wa VETA.
Mkutano huo umeandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Singida pamoja na Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Singida ( SISUPA) na kushirikisha Wadau wapatao 110 kutoka Mkoa wa Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...