Na.Khadija seif, Michuzi TV.
WALINZI
shirikishi pamoja na mabaunsa wametunukiwa vyeti baada ya Kumaliza
mafunzo yao ya ulinzi shirikishi kupitia Jeshi la Polisi (TPSIS)
Juma Gabriel ni mmoja wa Wakufunzi waliopatiwa mafunzo kutoka jeshi la polisi (TPSIS) nakutambulika kama mmoja wa walinzi shiriki.
Gabriel
amesema mafunzo hayo yanawapa wepesi wa kujitambua na kutambulika
kisheria tofauti na walinzi ambao jeshi la polisi haliwatambui pamoja na
weledi.
"Mafunzo hayo
yameweza kutupatia elimu ya ziada ambapo wengi wetu tulikua hatufahamu
pamoja na kitambulisho kitakachotusaidia kutambulika mbele ya jamii
pindi tuwapo kwenye doria ,"
Amezitaja
nafasi ambazo walinzi hao shiriki ufanya ikiwemo walinzi wa
makampuni,mlinzi wa mtu maarufu au Kiongozi haya yeye ni mlinzi wa
msanii Mbosso kutoka kundi la wasafi.
"Imenipa
fursa Sasa niweze kufanya kazi zangu kwa weledi na ufanisi kwani mwanzo
tulikua hatujawahi kuwekwa pamoja na kufanya mafunzo Kama hayo,"
Pia
ametoa pongezi kwa jeshi la polisi (TPSIS)kuiona fursa kwao kutoa
mafunzo hayo kwa baunsa hao ili kuwawezesha kutambulika kwa urahisi na
kuhalalisha kazi hiyo Kama kazi nyingine za kulinda mali ya umma na
wanajamii pamoja na kupewa mbinu nyingi za kikazi zaidi.
Kwa
upande wake Muhitimu wa mfunzo hayo Elias Masoud amesema muda wa
mafunzo hayo umekuwa ni wa siku tatu na amewaomba uongozi kuona fursa
nyingine kuongeza siku kwa awamu nyingine ili kujifunza zaidi.
"Mafunzo
yanatija sana kwa jamii kwani majukumu ya kazi inakua rahisi kwa jeshi
la polisi kuwa pamoja na ulinzi shirikishi (Mabaunsa) na kufanya kazi
kwa pamoja,"
Pia ametoa
ushauri kwa wamiliki wa walinzi shiriki hao kuwapa nafasi kwenda
kujifunza mafunzo hayo kwa usalama wa mali zao pamoja na wao wenyewe kwa
ujumla.
Afisa Mnadhimu wa jeshi la polisi ACP.Janeth Magombi
akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki katika mafunzo ya ulinzi shirikishi
kwa walinzi wa makampuni pamoja mabaunsa waliopata mafunzo siku tatu
jijini Dar es salaam
Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki waliopatiwa
mafunzo ya siku tatu ya weledi kazini na kujitambua kutoka sekta binafsi
jeshi la polisi (TPSIS) wakiwa na Afisa Mnadhimu wa jeshi la polisi
ACP.Janeth Magombi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa sekta binafsi ya
kutow mafunzo ya ulinzi shirikishi (TPSIS) Dr. David Rwegoshora
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...