Waziri wa nchi Ofisi ya Rais –
TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Michezo wa Mikoa na
Halmashauri za Tanzania Bara waliohudhurua Kikao Kazi cha siku mbili (12
– 13,Desemba 2019) kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira
na Maendeleo ya Viwanda” wakati akifunga kikao hicho leo Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akitoa taarifa fupi ya
kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara
kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) wakati wa ufungaji
wa kikao hicho uliofanywa na Mhe. Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais – TAMISEMI Jijini Dodoma kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo
kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Bernard
Patrick akitoa ufafanuzi kuhusu Muundo wa Utumishi katika kada ya
Michezo kwa Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara
wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba
2019)kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo
ya Viwanda” leo Jijini Dodoma.
Dkt.Jonas Tiberoha akiwasilisha
mada ya “Masoko,Udhamini na Maandalizi ya Maandiko katika Michezo”
wakati wa kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za
Tanzania Bara kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019)
Jijini Dodoma kilichongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na
Maendeleo ya Viwanda”
………………..
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo
amewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanawawezesha
Maafisa Michezo katika ofisi zao kushiriki katika kikao cha mwakani.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo
jijini Dodoma alipokuwa akifunga Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa
Tanzania Bara ambacho kimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dodoma
kikilenga kuwajengea uwezo maafisa hao katika kusimamia masuala ya
michezo na kujitathmini na kupeana maelekezo ya nini kifanyike kuboresha
sekta ya michezo nchini.
“Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015
imejadili kwa upana agenda ya michezo na kwa kiongozi yoyote wa
serikali anayepinga suala la michezo ni mmoja ya watu wanaokwamisha
utekelezaji wa ilani kwani watumishi wa umma wanatekeleza ilani ya chama
kilichopo madarakani,’alisema Mhe.Jafo.
Akiendelea kuzungumza wakati wa
kufunga kikao kazi hicho Mhe.Jafo alisisitiza hivi karibuni baada ya
michezo kurudishwa mashuleni tumeshuhudia vijana wadogo wakifanya mambo
makubwa katika michezo mfano timu ya Serengeti Boys ambayo imekwenda
mpaka AFCON U17 halikadhalika ubingwa wa Copa Coca Cola mwaka huu, na
haya ni matokeo ya kazi za Maafisa Michezo katika kuibua vipaji hivi.
Aidha, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi alisistiza kuwa
tasnia ya michezo ni muhimu sana katika kukuza uchumi na ni moja ya
sekta inayotoa ajira nyingi kwa wanamichezo na ndiyo yenye watu
wanaongozwa kulipwa fedha nyingi hivyo sekta hii ikisimamiwa vyema
inaweza kulipeleka taifa mbali katika maendeleo.
“Nimatarajio yangu kuwa kikao kazi
hichi kitaleta matokeo chanya na maafisa hawa wataenda kusimamia vyema
michezo katika maeneo yao na kuondoa dhana potofu ya watu kudharau
michezo, pia wataibua vipaji vipya vya wanamichezo kama wanariadha
mahiri zaidi ya akina Philbert Bayi,Suleiman Nyambui na Mwinga Mwanjala.
Tanzania ina watu wengi sana na tuna uwezo wa kuibua vipaji vikubwa
vitakavyo leta medali za dhahabu” alisema Dkt.Possi.
Pamoja na hayo Dkt.Possi
alisisitiza kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya ambao miongoni mwao wapo
wengi wenye vipaji hivyo ipo haja maafisa michezo hao kuhakikisha katika
maeneo yao wanafanya kazi kubwa ya kuibua vipaji haswa kwa vijana kwani
hao ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Halikadhalika Afisa Michezo
kutoka Wilaya ya Siha Bibi.Neema Joseph alishukuru uongozi wa Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuandaa kikao kazi ambacho mbali
na kuwapatia elimu ya kuandaa maandiko ya kuomba ufadhili katika michezo
pia amejifunza mambo mengi ambayo alikuwa hayajui na hivi sasa wilaya
yake haitaenda kuwa kama ilivyokuwa awali kutoka na mafunzo aliyopata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...