


…………………………………………………..
Na Farida Ramadhani na Saidina Msangi WFM, Dodoma
Wizara ya Fedha
na Mipango imeahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu
wa mipango ili kuboresha usimamizi wa sera na mipango ya maendeleo ya
nchi.
Hayo yameelezwa
na Kamshina wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja
wakati wa kuhitimisha kongamano la Wanamipango kwa mwaka 2019
lililofanyika Jijini Dodoma.
Bw. Mhoja alisema
kuwa kongamano hilo limetoa mapendekezo muhimu ambayo yatasaidia
kuboresha upangaji na utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya
maendeleo nchini.
Aliwashukuru
washiriki wote kwa michango, mawazo na fikra pevu wakati wa kongamano
ambayo itasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu taaluma
ya mipango.
Naye Mchumi Mkuu
Wizara ya Kilimo Bw.Adam Msumule ,ambaye ni miongoni mwa washiriki wa
kongamano hilo amepongeza waandaaji wa kongamano hilo muhimu kwa ajili
ya kubadilishana uzoefu na kuboresha mipango ya nchi.
Bw. Msumule
alishauri kongamano hilo kufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa
wataalamu kufanya tathmnini ya mipango iliyopo, iliyotekelezwa na kuona
namna ya kuiboresha.
Kongamano hilo
lililokuwa na kauli mbiu ugharamiaji wa maendeleo, lilitoa fursa kwa
washiriki kujadili mawasilisho mbalimbali ikiwemo vyanzo bunifu vya
ugharamiaji mipango ya maendeleo ya Taifa, Sera, Sheria na mfumo wa
kitaasisi unaosimamia ugharamiaji wa maendeleo nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...