Baadhi ya Mihuri aliyokutwa nayo Mtuhumiwa ABRAHAM OBEDI
Kompyuta aina ya Accer aliyokutwa nayo ABRAHAM OBEDI
Mihuri na nyaraka mbalimbali za Serikali na binafsi aliyokutwa nayo mtuhumiwa wa kughushi
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ABRAHAM OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi
wa Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuri hamsini
na sita [56] ya idara mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo
imeghushiwa na kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.
Mtuhumiwa
alikamatwa Disemba 31, 2019 majira
ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya
Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la
Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa
kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.
Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo
mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
1. Mhuri
wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,
2.
Mhuri wa Afisa biashara
wa Halmashauri ya Mbeya,
3.
Access Bank Tawi la Mbeya,
4.
Mamlaka ya Mapato Mbeya
[TRA]
5. Hakimu
Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,
Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima,
Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao
vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
KUPATIKANA
NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia AGREY MASHAKA @ MBOTO [25] Mkazi wa Kilambo Wilayani Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi kavu kilogramu thelathini [30].
Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 14:45 mchana baada ya Jeshi la
Polisi Mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya
Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni
muuzaji na mtumiaji wa bangi hiyo.
Imetolewa
na:
[ULRICH
O. MATEI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...