Katika Hali isiyo ya kawaida Afisa tarafa wa Mchichira Wilaya ya Tandahimba Bi.Dotto Nyirenda amefanikiwa kuwavalisha viatu wanafunzi takribani 77 waliopo katika shule ya Msingi Mbuyuni iloyopo katika kata ya Maundo.

Bi Dotto Nyirenda alieleza kuwa awali mwaka Jana alishawahi kufanya ziara ya kampeni ya shule ni choo katika shule hiyo na alikuta takribani robo tatu ya wanafunzi hawana viatu hivyo aliahidi kuwasaidia watoto hao.

Akizungumza na mwandishi wa habari mmoja wa wanafunzi hao alieleza kuwa anatambua kuwa wazazi wake wanao uwezo wa kumnunulia viatu lakin hafahamu kwanini hawajafanya hivyo,Aidha ameeleza adha kubwa wanayopata wanafunzi wanapokuwa hawana viatu ama wanapoenda shuleni na ndala ni pamoja na kuchomwa na miba na wakati wanapoenda chooni inabidi wamuazime mwenzao mwenye viatu na wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda mrefu.

 Afisa tarafa wa Mchichira Bi Dotto Nyirenda amewakumbusha wazazi hao kuwa ili mwanafunzi aweze kuwa makini darasani ni pamoja na mavazi ikiwemo viatu hivyo amewahamisha wazazi hao kuwa na utaratibu wa kuwanunulia wanafunzi hao viatu pindi wanaponunua vifaa vingine vya wanafunzi hao.

Bi Dotto Nyirenda pia alichukua fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wa maendeleo ikiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kwa kuchangia zoezi Hilo.

Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na wanakijiji, wameeleza kuwa changamoto nyingine waliyokuwa nayo katika kijiji hicho ni kukosekana na mtandao pamoja na barabara mbovu isiyopitika vizuri.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...