Na Yassir Simba, Globu ya Jamii
Ligi kuu soka Tanzania bara (VPL) kuendelea kutimua vumbi leo katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam, ambapo timu ya Azam fc "wanalambalamba" watawakaribisha vijana wa mtaa wa Jangwani na Twiga, Timu ya Wananchi ya Yanga majira ya saa moja usiku.
Azam fc ambao wametoka kutakata katika mchezo uliopita mbele ya wanapaluhengo Lipuli fc ya mkoani Iringa kwa ushindi mnono wa goli 2-0, wametamba kuwaonyesha kazi wageni wao Yanga ambao walipoteza mchezo wao dhidi super nkurukumbi Kagera Sukari kwa mabao 3-0.
Kwa Upande wa Yanga, wamejinasibu kuwa watawaonyesha kazi wanalambalamba hao kwa kuwafunga mdomo kwa idadi kubwa ya magoli.
Mchezi huo wa leo unatazamiwa kuwa ni vuta nikuvute, huku takwimu ikionyesha katika michezo mitano ambayo timu hizo zimekutana, Azam fc ameshinda mara mbili huku Yanga akipata ushindi katika mara tatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...