Shilingi
Bilioni 23.5 zinaokolewa kila mwaka baada ya Serikali kupitia Shirika la umeme
Tanzania (TANESCO) kuzima mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Shirika hilo
katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano, Mkurugenzi
mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka amesema kuwa Shirika hilo
limefanikiwa kujiendesha bila kupokea ruzuku
kufuatia hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kuzimwa kwa mitambo
ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta.
“Tumezima
mitambo ya kuzalisha umeme kwa mafuta mazito katika maeneo ya Makambako, Tunduru, Liwale, Namtumbo, Ludewa,
Madaba na kuyaunganisha na gridi ya
Taifa hali inayochangia kuongeza kasi ya maendeleo katika maeneo hayo na
kupunguza gharama za uendeshaji ;” Alisisitiza Dkt. Mwinuka
Akitaja
baadhi ya mitambo iliyozimwa Dkt. Mwinuka amesema kuwa ni ile ya IPTL,
AGRECO, Syimbion na mingine katika maeneo mbalimbali hapa nchini
iliyokuwa ikitumia mafuta katika uzalishaji wa umeme.
Akifafanua
amesema kuwa hali hiyo imechangia katika kuongeza mapato ya Shirika hilo kutoka
Shilingi takribani trilioni 1.2 mwaka 2012 hadi kufikia zaidi ya trilioni 1.5 kwa
mwaka kwa sasa hali inayoliwezesha Shirika hilo kuendelea kuongeza tija katika
utoaji wa huduma.
Kwa upande
wa wateja waliounganishiwa umeme wameongezeka kutoka milioni 1.6 waliokuwepo
kufikia mwaka 2015 hadi zaidi ya milioni 2.7 kufikia mwaka 2019 sawa na
ongezeko la wateja zaidi ya milioni 1.05 katika kipindi hicho ambao ni asilimia
63.84.
Akizungumzia
miradi ya kimkakati Dkt. Mwinuka amesema kuwa ni pamoja na mradi wa kufua umeme
wa Mwalimu Nyerere katika Mto Rufiji megawati 2115 unaotekelezwa na Serikali
kwa gharama ya shilingi trilioni 6.55, Rusumo megawati 80, Kakono megawati 87,
Mradi wa kuzalisha umeme kwa gesi mkoani Mtwara megawati 300.
Akieleza
zaidi, Dkt. Mwinuka amesema kuwa miradi mingine inatekelezwa katika maeneo
mengine katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila
mwananchi anafikiwa na huduma ya umeme.
Kwa upande
wa Vijiji vilivyounganishiwa umeme vimeongezeka kutoka 2018 mwaka 2015 hadi Vijiji
8236 kufikia Desemba 2019 ikiwa ni ongezeko la asimia 67 hali inayotokana na
jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa
na nishati ya umeme katika maeneo yote.
Katika
kipindi cha miaka 4 umeme ulioongezwa kwenye gridi ya Taifa ni Megawati 400
zinazotokana na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo ya Kinyerezi namba 1
na namba 2.
“Kwa
upande wa wateja wa viwanda wameongezeka
kutoka 2571 mwaka 2015 hadi 3787 mwezi
Desemba 2019;” Alisisitiza Dkt. Mwinuka
Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) limetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya uzalishaji,
usambazaji na uwekezaji katika sekta ya nishati ili kukuza uchumi na ustawi wa
wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...