NA YEREMIAS NGERANGERA…..NAMTUMBO

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo amewataka wananchi kuacha kununua bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi na kuendelea kununua bidhaa ambazo zimeisha muda wake wa maatumizi ni hatari kwa afya za watumiaji.

Akizungumza na wafanyabiashara na wananchi wa soko la mji mdogo wa Namtumbo Kizigo aliwataka wananchi kujihadhari na kununua bidhaa zilizoisha muda wake na kufanya hivyo ni kuhatarisha afya za watumiaji .

Aidha mkuu wa wilaya aliwataka wafanyabiashara ambao ndio wenye bidhaa hizo kuwauzia wateja bidhaa ambazo hazijaisha muda wake na kuwataka wafanyabiashara hao kubandika matangazo katika maduka yao kuwatangazia wateja wao kuwa kabla ya kununua bidhaa wahakikisha wanasoma muda wa kuisha matumizi kwa bidhaa wanazonunua alisema mkuu wa wilaya huyo.

“Tutapita kwenye maduka yote Wilaya nzima kuona agizo la kubandika tangazo la kuwataka wateja wenu wanunue bidhaa zisizoisha muda wake kwenye maduka yenu limetekelezwa na ninyi wenye maduka kutouza bidhaa zilizoisha muda wake linatekelezwa “alisema mkuu wa wilaya huyo.

Afisa afya wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Elias Boniface katika taarifa yake kwa mkuu wa wilaya huyo alidai kamati ya ukaguzi ya wilaya ilikagua maduka Wilayani humo kwa awamu tatu pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kuepuka kununua bidhaa zilizoisha muda wake na kueleza madhara ya kununua bidhaa zilizoisha muda wake kwa wananchi.

Bwana Boniface katika taarifa hiyo alisema kamati hiyo ilibaini wananchi wakifika dukani hawana muda wa kuuliza au hawana uelewa wa maswala ya bidhaa kama yana muda wake rasmi wa matumizi badala yake wao wanaangalia kununua na kutumia.

Pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji na wafanyabiashara afisa afya huyo katika taarifa hiyo waliwaeleza wananchi kutoa taarifa kwa mfanyabiashara yeyote anayeuza bidhaa zilizoisha muda wake kwa kuwa wafanyabiashara hao wamisha elekezwa kutouza bidhaa zilizoisha muda wake kwa watumiaji na kufanya hivyo ni kosa kisheria alisema afisa afya huyo.

Sadiki Zuberi Ally mkazi wa Namtumbo alikutwa na mkuu wa wilaya akiwa amenunua bidhaa ya maziwa katika duka moja wapo hapa Namtumbo na alipoulizwa na mkuu wa wilaya kuhusu bidhaa hiyo inaisha muda wake lini hakuweza kujibu swali hilo na kudai kuwa yeye amenunua anajua ni salama kwa kuwa zimeruhusiwa kuuzwa na hana kawaida ya kusoma muda wa kuisha muda kwa bidhaa hiyo.

Hata hivyo bwana Sadiki alishukuru kupatiwa elimu na kuambiwa kuwa maziwa aliyonunua yanaisha muda wake tarehe 21 februali mwaka huu na yeye kujisomea eneo lililoandikwa tarehe hiyo na kuhaidi kununua bidhaa kwa kuangalia muda wa matumizi ya bidhaa yoyote atakayonunua.

Serikali Wilayani Namtumbo imedhamiria kuwachukulia hatua za kisheria pamoja na kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara watakaobainika kuuza bidhaa zilizopita muda wake kwa kukaidi agizo la serikali la kuwataka kutouza bidha hizo katika maduka yao.

 
Dc akiwa katika moja ya duka katika mji mdogo wa Namtumbo kukagua bidhaa zilizoisha muda wake
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...