MWANAMITINDO maarufu Duniani Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Marekani,Flaviana Matata ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii akiwa ameambatana na Wanamitindo wenzake kutoka Marekani.
Flaviana Matata ameongozana na wanamitindo hao akiwemo: Shelby Colemans, Daniella Evans na Awa Florence Mafany ambao kila mmoja anafanya shughuli za mitindo huku wakiwa na wafuasi wengi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Flaviana Matata akiwa na rafiki zake hao, wameweza kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya Serengeti ikiwemo wanyama mbalimbali sambamba na uzuri wa Hifadhi hiyo ambayo ni kubwa hapa Nchini.
Ziara hiyo ya kuambatana na Wanamitindo hao ni kwa lengo la kuona vivutio vya utalii vilivyoko katika hifadhi na kuvitangaza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...