SHULE
ya awali na msingi Glisten International ya Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara imezidi kufagiliwa kwa kuongoza kwa
ufaulu wa matokeo ya darasa la nne kwa mkoa huo.
Shule
ya Glisten kwa mujibu wa matokeo ya darasa la nne ya mwaka 2019
imeshika nafasi ya kwanza kwa Wilaya ya Simanjiro, ya kwanza pia kwa
mkoa wa Manyara na ya 39 kitaifa kwa shule zote za msingi 3,244 za
Tanzania.
Mkurugenzi wa
shule ya Glisten, Justin Mirisho Nyari alisema anawazawadia walimu wanne
waliowafundisha wanafunzi wa darasa la nne wa mwaka jana shilingi laki
moja kila mmoja kama zawadi ya matokeo hayo.
Nyari
ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara
(Marema) na mheshimiwa diwani mstaafu wa Kata ya Mirerani aliwaahidi
wanafunzi 30 wa taaluma ya michezo kuwanunulia sare za michezo kutokana
na vipaji walivyonavyo.
Alisema
lengo la kuanzisha na kuwekeza kwenye shule hiyo iliyopatiwa usajili
mwaka 2017 ni kuhakikisha watoto wa eneo hilo wanapata elimu bora.
"Tunamuunga
mkono Rais John Magufuli kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu kwani
tumeona juhudi zake za kusimamia maendeleo ikiwemo kujenga ukuta
unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite ili kulinda rasilimali hiyo
muhimu," alisema.
Ofisa
elimu ya watu wazima wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Lazaro
Tibaigana aliwataka walimu na wanafunzi wa shule hiyo kutobweteka na
ushindi huo kwani shule nyingine nazo zinalengo la kushika nafasi ya
kwanza kimkoa.
"Mmetupa
heshima kubwa wilaya ya Simanjiro kwa kuongoza kwenye mkoa wa Manyara
hivyo kazeni buti zaidi ili muongoze tena," alisema.
Mmoja
kati ya wanafunzi wa shule hiyo Magreth Leons Kimario alisema
wanamuombea Mkurugenzi wa shule hiyo Justin Nyari kwa Mungu ili aweze
kuendeleza shule yao.
"Pia
tunawaombea walimu na wazazi wetu waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo
na kusababisha sisi tofauti mitihani yetu kupitia masomo
tunayofundishwa," alisema.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Sabato Joshua alisema katika tafrija hiyo wanafunzi
wa darasa la nne wa mwaka jana walipatiwa zawadi ya vyeti na vitabu kwa
kila somo walilochagua.
Hata
hivyo, ili kuonyesha umoja na upendo, baadhi ya walimu wa shule ya
awali na msingi New Vision ya mji mdogo wa Mirerani, walishiriki pamoja
kwenye tafrija hiyo.
Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Glisten
International ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, Justin
Mirisho Nyari ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini
Mkoa wa Manyara (Marema) akizungumza wakati akiwapongeza wanafunzi
walioongoza mtihani wa darasa la nne mwaka jana ambapo shule hiyo
ilishika nafasi ya kwanza kimkoa, nafasi ya 39 kitaifa kati ya shule
3,244 zilizopo nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...