Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kuwaonywa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya mauaji yanayotokana na imani za ushirikina na kwamba amesisitiza kuwa, suala la amani ni la umuhimu hususani kwa maendeleo ya taifa.
IGP Sirro amesema hayo akiwa Kakola Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo ambapo ameitaka jamii kushirikina na vyombo vya dola katika kuhakikisha suala la amani linaendelea kudumishwa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kakola Kilikili James amesema kuwa, wapo watu wanaofahamika ambao wamekuwa wakijihusisha na ramli chonganishi na hivyo wapo tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyohuzika ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...