Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga muda mfupi alipowasili katika mkoa huo kwa ajili ya ziara ya kikao kazi chenye lengo la kukutana na Makamanda wa Polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Simiyu ili kuweka mikakati ya pamoja katika kushughulikia makosa ya mauaji yanayojitokeza nchini. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amekutana na Makamanda wa Polisi  wa mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuweka mikakati na mpago kazi wa pamoja katika kushughulikia matukio ya mauaji yanayojitokeza nchini ikiwa ni pamoja na kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kuwakamata na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akiwa mkoani Shinyanga IGP Sirro, amewaonya wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya imani za kishirikina vinavyopelekea mauaji yanayotokana na imani hizo na badala yake kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kuwafichua wahalifu.

Aidha, IGP Sirro amemuagiza Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Nchini CP Liberatus Sabas, na Makamanda wote wa mikoa ya Shinyanga, Geita, Kagera, Mwanza na Simiyu kufanya operesheni ya pamoja itakayosaidia kukomesha vitendo vya mauaji nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...