Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani akitoa taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu na
upatikanaji wa fedha katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika
kipindi cha nusu mwaka wa 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani akitoa taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu na
upatikanaji wa fedha katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika
kipindi cha nusu mwaka wa 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Watendaji wa Taasisi zilizo chini
ya Wizara ya Nishati, wakiwa katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini. Kikao hicho kililenga kutoa taarifa ya Wizara
kuhusu utekelezaji wa majukumu na upatikanaji wa fedha katika Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya
Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika kipindi cha nusu mwaka wa
2019/2020 kilichofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula akizungumza jambo katika
kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara ya Nishati na Taasisi zake
kilicholenga kupata taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu na
upatikanaji wa fedha katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika
kipindi cha nusu mwaka wa 2019/2020. kushoto kwake ni Katibu wa Kamati
hiyo, Felister Mgonja.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato
Kabaka akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
kuhusu utekelezaji wa majukumu na upatikanaji wa fedha katika kampuni
hiyo katika kipindi cha nusu mwaka wa 2019/2020.
………………..
Na Teresia Mhagama, Dodoma
Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Nishati na Madini, kupitia Mwenyekiti wake, Dunstan
Kitandula imewapongeza viongozi wa Wizara ya Nishati, kwa usimamizi wao
unaoendelea kuboresha utendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
kuhakikisha kuwa Shirika hilo linatekeleza majukumu yake ipasavyo na
kutoa huduma bora kwa wananchi.
Pongezi hizo
zimetolewa tarehe 18 Januari, 2020 jijini Dodoma wakati wa kikao cha
Kamati hiyo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake
wakiongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu.
Kikao hicho
kilikuwa mahsusi kwa ajili ya utoaji wa taarifa ya Wizara kuhusu
utekelezaji wa majukumu na upatikanaji wa fedha katika Shirika la Umeme
Tanzania na Kampuni ya Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi Tanzania
(TGDC) katika kipindi cha nusu mwaka wa 2019/2020.
“ Tunaona
jitihada zinazofanyika za kuiboresha TANESCO na sisi tunakupongeza
Waziri na timu yako, lakini bado kuna vitu vya kurekebisha ikiwemo
kuwafanya baadhi ya watumishi wa TANESCO kutoka kwenye ufanyaji kazi wa
kimazoea unaotokana na kuona kuwa Shirika hili ni la umma na wawe na
mtazamo wa kibiashara ambao utaliletea faida Shirika huku likitoa huduma
bora kwa wananchi.” Alisema Kitandula
Kitandula pia
alisisitiza kuwa, kasi ya kuunganisha wananchi na huduma ya umeme
iongezeke pamoja na uboreshaji wa utoaji wa taarifa kwa wananchi
akitolea mfano kuwa, inapotokea changamoto ya umeme, wananchi wapewe
taarifa ndani ya muda muafaka na kuwe na mawasiliano chanya kati ya
mteja na watoa huduma wa TANESCO.
Aidha, Kamati ya
Bunge iliipongeza TANESCO kwa kuacha kutegemea ruzuku kutoka serikalini
ili kujiendesha na kwa mara ya kwanza imetoa gawio serikalini la
shilingi bilioni 1.436 katika mwaka 2019.
Kuhusu TGDC,
Kamati iliipongeza kampuni hiyo kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa
Jotoardhi inaendelezwa na kusema kuwa kampuni hiyo ni muhimu katika
uendelezaji wa rasilimali hiyo ambayo ni moja ya vyanzo vya nishati
jadidifu nchini na itawezesha juhudi za Serikali za kuwa na umeme wa
uhakika kwani Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme wa Jotoardhi
usiopungua megawati 5000.
Waziri wa
Nishati, awali, alipata fursa ya kueleza hali ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme ambapo katika
uzalishaji umeme alisema kuwa uwezo wa mitambo ya kufua umeme nchini
umefikia jumla ya megawati 1,602.318 huku mahitaji ya juu katika mfumo
wa gridi ya Taifa yakifikia megawati 1,120.12 ambayo yalifikiwa tarehe
27 Novemba, 2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...