Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa
na Michezo Balozi Ali Abeid Karume akisisitiza jambo wakati akitoa
hotuba ya Ufunguzi wa Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni
Zanzibar.

Baadhi ya wananchi na Waalikwa
mbalimbali waliohudhuria Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni
Zanzibar.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga akitoa hotuba ya kumkaribisha
mgeni Rasmi katika Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni
Zanzibar.

Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa
na Michezo Baloz Ali Abeid Karume akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Kongamano
la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa
Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.

Mtoa mada Nd,Ali Shaaban akitoa
mada kuhusu Maisha ya Sheikh Abeid Amani Karume katika Ufunguzi wa
Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika
Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.

Mtoa mada Mshauri wa Rais wa
mambo ya Kale na Historia Ali Mzee Ali akitoa mada kuhusu Mapinduzi ya
Zanzibar na Maendeleo katika Ufunguzi wa Kongamano la miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss
Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
………………
Na Mwashungi Tahir,Maelezo.
WAZIRI wa Vijana,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume amesema Serikali
itaendelea kuwaelimisha vijana na kuhakikisha kwamba wanayaenzi na
kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.
Ameyasema hayo
wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Miaka 56 ya Mapinduzi ya
Matukufu ya Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya Mapinduzi
hayo lililofanyika huko katika ukumbi wa Idrissa Abdul Wakil huko
Kikwajuni.
Amesema vijana
wanapaswa kuifahamu Historia ya nchi yao kwa lengo la kuyajua mambo
yaliyotokea kabla ya Mapinduzi hadi kupatikana kwa uhuru na kujikomboa.
“Vijana kongamano
hili litaweza kuona historia ya Mapinduzi tangu yalivyoanzia hadi
kufikia kupata uhuru wa Nchi yetu”alisema Waziri Karume.Alieleza kuwa
wananchi ni vyema kuwakumbuka waasisi waliofanya Mapinduzi chini ya
uongozi wake Jemedari Mkuu Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
aliyemkomboa Mzanzibar katika makucha ya kisultani na kumpatia uhuru.
Balozi Ali Karume
alisema kuwa Lengo la kongamano hilo kuwaelimisha vijana na kuijua
historia ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi pamoja na kumfahamu
mwasisi Marehemu Mzee Karume jinsi alivyopigana na kuleta maendeleo
nchini.Aidha Balozi
Karume alimpongeza Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wa awamu
zilizopita kwa kuyaendeleza yale yote yaliyoasisiwa na marehemu Mzee
Karume na kuleta maendeleo pamoja na kudumisha amani na utulivu nchini.
Balozi Karume
aliwataka vijana hao kutosikiliza maneno ya wasiopenda maendeleo kwani
Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika kihalali chini ya Jemedari Mkuu
Marehemu Mzee Karume.
Mada mbili
ziliwasilishwa ikiwemo Maisha ya Marehemu Mzee Karume na Mada ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Maendeleo ambapo Mshauri wa Rais katika mambo
ya Historia na Mambo ya Kale Ali Mzee Ali, aliiwasilisha kwenye
kongamano hilo linalo lengo la kuwaenzi wazee walojitolea muhanga
katika kupigania uhuru kw a kumng’oa mkoloni na kupata maendeleo
nchini.
Aidha
aliwasisitiza vijana kuyaenzi Mapinduzi na kuyathamini kwani yameweza
kuletea maendeleo kwa kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya,
maji safi na salama na miundombinu nchini.
“Mapinduzi ya
Zanzibar yametuletea maendeleo makubwa hivyo ni vyema yazidi kuendelezwa
kutunzwa na kuthaminiwa”, alisema Mshauri huyo.
“Vijana
nawaombeni kufuata wasia aliyouacha Marehemu Mzee Karume kwamba tukuza
kilicho chako na kusahau cha mwenzako, poteza maisha yako kwa kuokoa
nchi yako”, alieleza Mshauri huyo
Nae Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Mjini Talib Ali Talib alishauri kutolewa
kwa elimu ya Historia ya Zanzibar kwa vijana ili kuweza kutambua mambo
yote yaliyotokea nchini.Pia aliwataka
wasanii kufikisha ujumbe wa mambo yaliyotokea kabla ya Mapinduzi hadi
kupatikana uhuru wa Zanzibar kupitia michezo ya kuigiza ili jamii iweze
kufahamu historia ilikotoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...