
Ingawa
hakuna vyanzo vya kutosha juu ya maisha ya Utotoni ya Shaaban Robert
lakini masimulizi yanaeleza alianza kazi kama Karani kwenye Serikali ya
Kikoloni mara baada ya kumaliza Darasa la 11. Ndani ya Serikali ya
kikoloni alihudumu kama Karani, Afisa forodha(Bandari za Pangani na
Bagamoyo), Ofisa-Mbuga ya Wanyama, Ofisi ya Vipimo na Ramani na hatimaye
Idara ya Mipango!
Kwa nyakati tofauti alioa, wake watatu. Na kujaaliwa watoto kadhaa.
Pengine
Shaaban Robert ndio mtunzi mashuhuri zaidi wa kazi za Fasihi ya Lugha
ya Kiswahili. Aliandika Miswaada mbalimbali ya Mashairi, Insha na
Riwaya(Mpaka hivi karibu, barua na insha zake zinachapishwa).
Anajulikana kama Shakespeare wa Fasihi ya Kiswahili.
Miaka
58 baada ya Kifo chake bado kazi zake zinaakisi maisha ya sasa. Jina
lake limebaki kwenye miadhara ya lugha ya Kiswahili na Magazetini.
Ingawa
aliandika tangu miaka ya 1920 lakini kazi yake ya kwanza ilitoka katika
gazeti "Mamboleo" mwaka 1932, ikiwa ni barua kwa Mhariri wa Gazeti
hilo, kazi hii iliitwa "Hirizi ya shilingi Mia" katika Barua hii Shaaban
Robert alikemea tabia za Ushirikina au Shirki
Shaabani
Robert alifariki Dunia, tarehe 22-06-1962 kwa Ugonjwa wa Moyo na
kupungukiwa Damu akiwa na Umri wa Miaka 53 tu. Alizikwa Kijijini kwao
Vibambani, Tanga.
Baadhi ya kazi alizoziandika au kuzitunga na kuacha Miswaada ni.....
1.Almasi za Afrika ( 1971)
2.Koja la Lugha(1969)
3. Insha na Mashairi(1967)
4.Kielezo cha Fasihi(1962)
5. Pambo la Lugha(1968)
6.Ashiki Kitabu Hiki (1968)
7. Mashairi ya Shaaban Robert (1971)
8. Sanaa ya Ushairi(1972)
9. Mwafrika Aimba(1969)
10. Masomo yenye Adili (1959)
11.Mapenzi bora(1969)
12.Tenzi za Marudi Mema na Omar Khayyam (1973)
13. Utenzi wa Vita vya Uhuru (1961)
14. Almasi za Afrika na Tafsiri ya kiingereza (1960)
15. Maisha yangu na baada ya miaka hamsini(1949)
16. Adili na Nduguze(1977)
17. Kusadikika (1951)
18. Kufikirika(1968)
19.Wasifu wa Siti Binti Saadan(1967), binafsi nakipenda sana hiki kitabu!
20. Utu Bora Mkulima (1968)
21. Siku ya Watenzi wote(1968)
22. Barua za Shaaban Robert (1931-1958(2002)
23. Kielezo cha Insha(1954)
24. Methali na mifano ya kiswahili (2007)
Baada ya Kifo chake, Rais wa Tanganyika (wakati huo) aliutangaza mtaa wa Burton Street kuitwa Mtaa wa Shaaban Robert mwaka 1963.
Shaaban Robert ametunukiwa Tuzo na Vyeti mbalimbali kutokana na mchango wake kukuza fasihi na lugha ya Kiswahili.
Pamoja
na Uwezo wake wa kuchagua maneno na msamiati bora wa Kiswahili lakini
pia Shaaban Robert alikuwa na ujuzi mkubwa katika kuandika Lugha ya
Kiingereza. Ushaidi wa Barua alizoandikia rafiki zake unadhihirisha
hili.
Hivyo basi,
tunaposisitiza Matumizi ya Kiswahili tusisahau Kiingereza kwani Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipata kusema "Kiingereza ndio Kiswahili
cha Ulimwengu"
Kheri ya Mwaka Mpya!
Francis Daudi
0768035253
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...