Mwenyewe atoa kauli nzito, apinga kuondolewa kwake...sasa kudai Umeya wake mahakamani

Na Said Mwishehe

AMENG'OKA!Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kumemuondoa Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita katika nafasi yake kutokana na kupiga kura ya kutokuwa na imani naye huku vurugu kubwa zikiibuka mkutano na kusababisha baadhi ya wajumbe kutwangana makonde hadharani tena 'Live'.

Baada ya Mwita kuondolewa mzozo mkali uliibuka kati ya wajumbe wanaotoka upande wa upinzani na wale wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kiasi cha mmoja wa madiwani wa Chadema Patrick Asenga kukamatwa na Polisi kwa kile kinachodaiwa kusababisha fujo baada ya kuondolewa kwa Meya huyo.Ilikuwa kama filamu vile kumbe ndio Meya anaondoka hivyo.

ILIKUWA HIVI

Kikao cha kujadili na hatimaye kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya Mwiat kilianza saa tano asubuhi na wajumbe walikataa Mwita kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho kwa madai kuwa tuhuma zilizokuwa zinajadiliwa zilikiwa zikimhusu yeye,hivyo asingeweza kukiongoza vizuri.

Hivyo basi Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam alipewa jukumu la kusimamia kikao hicho ambacho kimeendeshwa kwa lisaaa limoja huku wajumbe akiwemo Mwanasheria wa Jiji akitoa ushauri wa kisheria kuhusu mchakato huo ambapo alishauri iadha ipigwe jura ya vikaratasi au mjumbe mmoja kutoa hoja ya kutokuwa na imani na Meya na kama ulikubaliwa ataondolewa moja kwa moja.

Hivyo wajumbe wa baraza hilo waliamua kufuata ushauri wa mmoja ya wajumbe kutoa hoja ya kutokuwa na imani na Meya ambapo wajumbe walisimama kuiunga mkono na hivyo kukubaliwa na kusababisha Mwita kuondolewa kwenye nafasi yake.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kumuondoa kwani Meya Mwita na wote wanaomuunga mkono kusimamia imara wakipinga kinachoendelea ,hata hivyo walizidiwa nguvu.

UNAJUA NINI KILICHOFUATA?


Diwani wa Kata ya ameondolewa kwenye nafasi yake na baraza la Halmashauri ya Jiji hilo baada ya kupita kura ya kutokuwa na imani naye kutokana na tuhuma tatu zinazomkabili ikiwemo ya matumizi mbaya ya ofisi.

MWANZO WA MCHEZO

Mwita wakati wa kikao hicho kimeanza alisema hawezi kukubali kikao Kianze bila kuwepo kwa wajumbe wa upande wa upinzani ,hivyo baadae wajumbe wake waliokuwa kikao nikaanza ingawa kwa malumbano makubwa yalitawala mkutanoni ambapo wapinzani hawakuwa wameridhika na kikao hicho.

Kutoka na mazingira hayo vurugu nikaanza kuibuka wakati wote kati ya madiwani wa upinzani na wale wa CCM.Pamoja na mambo mengine moja ya sababu ya malumbano na vurugu ziliibuka baada ya baadhi ya madiwani wa Chadema kudai baadhi ya wajumbe wa CCM hawamo ukumbini lakini majina yao yamo kwenye orodha ya waliohudhuria, hivyo mzozo ukaanzia hapo.Kila upande ukitoa maneno majali dhidi ya upande mwingine.

KAULI YA MWITA

Akizungumza baada ya kikao hicho kilichotangaza kumuondoa Isaya Mwita amewaambia waandishi wa habari kuwa maamuzi maamuzi hayo yamekosa nguvu kisheria kwani wajumbe waliopiga kura akili haijatimia hasa kwa kuzingatia ili uamuzi ufanyike unahitaji mbili ya tatu ya wajumbe ,ambayo haikufikiwa.

Amesema kikao cha leo kilikuwa na wajumbe 16 tu na waliokubali yeye aondolewe walikuwa wajumbe 13,wawili wamekataa na mmoja aliondolewa kikaoni,hivyo ili yeye aondolewe walipewa kuwemo wajumbe 17 lakini mmoja hakuwepo.

"Mimi bado ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam maaan utaratibu uliotumika ni batili na haujafuata taratibu za kisheria ambazo ziko wazi kabisa.Naomba Rais aingilie kati,ili haki iweze kupatikana.

"Niliwahi kusema hapo nyuma viongozi wa dini waniombee kwani napita kwenye wakati mgumu na leo mmeona kilichofanywa dhidi yangu.Kwa kuwa sijaridhika nakwenda Mahakamani kudai haki yangu.Ni aibu kilichofanyika na hata gari niliyokuwa naitumia nimenyang'anywa,"amesema Mwita.

ALICHOKISEMA MEYA TEMEKE

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Temeke amesema miongoni mwa tuhuma ambazo Mwita anatuhumiwa nazo na moja ya tuhuma ni kuwaingiza Mameya wa Manispaa zote tano za Jiji la Dar es Salaam katika Kamati ya fedha ,na hapo ni kinyume na kanuni na hapo ukiangalia itabaini kila mwaka Jiji limekuwa likipoteza milioni sita kila mwaka kwa kuwalipa posho wajumbe ambao wakaingia kinyume utaratibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...