Jeshi
la Polisi Mkoani Mwanza limemkamata na linaendelea kumshikilia mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Hemed Jumanne (40) mkazi wa Sengerema,anayedaiwa kuwa
Mganga wa Kienyeji,kwa tuhuma za kumbaka Mwanamke mmoja (jina kapuni) (32)
mkazi wa Butimba
Tukio
hilo limetokea Januari 4,2020 katika mtaa wa Jiwe,Kata ya Igogo Wilaya ya
Nyamagana,hii ni baada ya Muathirika wa tukio hilo kufika kwa Mganga Tajawa
hapo juu kwa lengo la kupata tiba ya maradhi yanayomsumbua,ndipo Mganga huyo
aliingiwa na tamaa ya Kimapendi na baadae alimpa dawa za kumpumbaza kisha
kumbaka kwa kuweka baadhi ya dawa za
Kienyeji sehemu za siri za Mwanaume
(Mganga) na baadae kuingiza sehemu za siri za Mwanamke kama sehemu ya matibabu.
Kitendo
hiki cha kikatili cha kubaka hakivumiliki,ni cha Kinyama na ni kosa la Jinai.
Mtuhumiwa
huyo atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,na Muathiriwa tukio hilo
ametibiwa hospitali na hali yake inaendelea vizuri,kwani ameruhusiwa kutoka.Jeshi
la Polisi linatoa wito kwa Wananchi kujiepusha na Makundi ya Wahalifu wanaotumia Mwamvuli wa Uganga wa Jadi
kutapeli Watu na kufanya vitendo vingine vya kijinai
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...