Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (katikati ) akiwasili katika eneo la kiwanja panapojengwa Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika eneo la Philips jana Jijini Arusha,wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbaro,na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano katika Sekta ya Mawasiliano Dkt.Jimmy Yonazi.

7:Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Posta Afrika huo mara kumalizika Mkutano Mkuu wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) yaliyofanyika jana Jijini Arusha,wanne kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye ndiyo aliyekuwa mgeni rasmi mkutano huo,wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika Bw.Younouss Djibrine na wapili ni kulia ni Kiongozi wa Umoja wa Afrika Bw.Cheikh Bedda.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika mkutano wa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za makao makuu ya Umoja wa Afrika Posta (PAPU)wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya umoja huo zilizofanyika jijini Arusha jana, aliyeketi wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akipongezaWaziri wa Ujenzi,Uchukuzi, na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe mara baada ya kuweka jiwela msingi wa kuwa la msingi kwa ajili la ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika
zoezi hilo limefanyika jana jijini Arusha.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wanne kulia)akifuatilia maelezo ya namna jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika litakavyokuwakutoka kwa mmoja wa wataalamu wa usimamizi wa Ujenzi wa jengo hilo (jina lake halikufahamika) kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi uliyofanyika jana Jijini Arusha, wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wapili kulia).

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika Younouss Djibrine ( kulia) wakati wa Sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika zinazojengwa jijini Arusha eneo la Philips.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...