Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa 
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Matias Haule akitoa 
ufafanuzi kuhusu maambukizi ya mapya ya UKIMWI kwa wanafunzi wa Shule ya
 Msingi Mininngani iliyoko Kondoa Mjini Mkoani Dodoma.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi 
Miningani iliyoko nje kidogo ya mji wa Kondoa wakisiliza kwa amakini 
mafunzo ya maambukizi ya UKIMWI kwa Vijana jana Kondoa Mkoani Dodoma.
*******************************
Na mwandishi wetu Kondoa
Wazee Wilayani 
Kondoa wameiomba Serikali kudhibiti picha zenye maudhui ya ngono katika 
mitandao ya Kijamii kwa lengo la kusaidia kupunguza maambukizi mapya ya 
UKIMWI kwani picha hizo zisizo kuwa na maadili zinawachochea 
vijana  kujiingiza katika matendo yanayosababisha maambukizi ya UKIMWI.
Wazee hao 
waliyasema hayo wakati wa mafunzo ya Siku moja kwa wazee wa mila pamoja 
na viongozi wa dini yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya Idara Kuu 
Maendelepo ya Jamii kwa lengo la kuwafundisha kuhusu  ukubwa watatizo la
 UKIMWI kwa vijana na kuwataka kusaidia kupambana na tatizo hilo katika 
jamii kupitia nafasi zao.
Mzee Mohamed 
Hussein Kola akitoa maoni yake katika kikao hicho alisema hata Siku 
mmoja hakuna mtu aliyefikishwa mbele ya sheria kwa mtu kuambukiza 
mwenzake UKIMWI kwa makusudi pamoja na uwepo wa sheria ya UKIMWI hapa 
Nchini.
Mzee Kola 
anaangazia pia suala la malezi na kusema kwamba vijana hawaeshimu tena 
mawazo ya wazee na kudai kuwa kila mzee akitoa maoni yake vijana 
wanasema mawazo ya mzee nayo yamepitwa na wakati na kudai kuwa hata kwa 
baadhi ya mafunzo ya magonjwa mbalimbali yanapotolewa wazee wamekuwa 
hawashirikishwi.
Mzee Haruna 
Ramadhani Dodi pia aliongeza kuwa vijana wadanganyana kupuuza uwepo wa 
maambukizi ya UKIMWI na kudai kuwa watakufa kishujaa uku akiwataka 
kupuuza mawazo haya kwani hakuna mtu aliyewai kufa kishujaa na kuonya 
pia juu ya uwepo wa maeneo ya biashara za kumbi za starehe kuwa 
zinachangia uwepo wa maambukizi. 
Taarifa hizi kwa 
wazee hao zilikuwa za kushtua kwani idadi ya maambukizi kwa vijana 
inazidi kupaa na hii ilizibitishwa na Afisa Maendeleo Mkuu kutoka Wizara
 ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Matias Haule aliyesema kuwa 
watanzania 200 wanapata maambukizi mapya kwa siku.
Aidha Bw. Haule 
alitoa takwimu hizo na kuongeza kuwa maabukizi haya kwa mwaka ni kiasi 
cha watu elfu 72 akiitaja idadi ya watu inayoambukizwa kwa mwezi kuwa 
watu elfu 6,000 na kushangaza wazee hao kwa kusema kwa vijana wenye umri
 kati ya miaka 15-24 maambukizi mapya kwao 79 na kati yao wasichana 
wanaombukizwa ni 63 hivyo idadi kubwa ya wasichana inaambukizwa 
ukilinganisha na wavulana.
Wizara ya Afya 
Maendealeo ya Jamii kwa Kushirikiana na TACAIDS pamoja na Shirika la 
TASAF wako Mkoani Dodoma kutembelea wasichana barehe na wanawake vijana 
pamoja na Shule mbalimbali Mkoani humo kwa lengo la kuhamasisha vijana 
juu yatishio jipya la maambukizi ya UKIMWI kwa vijana na zoezi hili 
litaendelea kwa Mkoa wa Morogoro na baadae Nchi Nzima.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...