


Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dorothy Nyanda akiwaeleza wafanyakazi wenzake kuhusu albamu yake mpya iitwayo Kristo Seba Waajuka (Bwana Yesu amefufuka) aliyoizindua mwishoni mwa mwaka jana akiwa na malengo ya nusu ya mauzo ya albamu hiyo kutumika kulipia gharama za matibabu ya moyo kwa watoto ambao familia zao hazina uwezo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Mohamed Songoro akisoma taarifa ya utendaji kazi wa kurugenzi hiyo katika kikao cha wafanyakazi wa JKCI kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.



Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kufungua mwaka cha wafanyakazi hao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.(PICHA NA JKCI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...