Na Daniel Mwambene, Ileje DC
“MICHANGO ya wananchi kwenye miradi ya ujenzi si pesa tu, pokeeni hata vitu vingine zikiwemo hata nguvu zao zithamanisheni”, RC wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela.
“MICHANGO ya wananchi kwenye miradi ya ujenzi si pesa tu, pokeeni hata vitu vingine zikiwemo hata nguvu zao zithamanisheni”, RC wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela.
Alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya siku moja ya kufungua shule za msingi na sekondari baada ya mapumziko ya mwezi mmoja akiangalia mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2020.
Katika ziara hiyo aliweza kutoa mifuko 80 ya saruji kwa shule nne za sekondari alizotembea ambazo ni Mbebe, Kakoma,Nakalulu na Itumba kila moja ikitarajia kupokea mifuko 20.
Akizungumza na katik Kata ya Mbebe RC Mwangela alisema kuwa kumekuwa na dhana potofu kwa baadhi ya viongozi na wananchi kuwa michango inayochangwa na wananchi baada ya kukubalina ni pesa tu hali aliyoipinga akisema ni upotoshaji.
Alisema kuwa,mwananchi anaweza kuchangia nguvu zake au vifaa vya ujenzi kama vile mbao na matofali na vitu hivyo havina budi kuthamanishwa ili kupata gharama za mradi.
Akizungumzia suala la kukamilisha majengo alisema viongozi hawana budi kukaa pamoja kwenye serikali za vijiji na kata katika kapanga mikakati ya ujenzi wa shule badala ya kusubiri kwanza matukio ya watoto kufaulu.
Kiongozi huyo aliweza kufurahishwa na uongozi wa Kata ya Isongole kwa jinsi wanavyoshirikiana na kuiweka wazi mipango yaujenzi wa shule huku akiutaka uongozi wa Kata ya Itumba na mambo yanavunja umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi.
Kwa upande wao walimu walimweleza kiongozi huyo kuwa walishajipanga kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ikiwemo kutumia vyumba vya akiba vilivyokuwepo pamoja na vyumba vya maabara kwa muda.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbebe Ndg.Yusuph Abdalah Tumbo akitoa maelezo
kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Nicodemas Mwangela kuhusu jinsi
walivyojipanaga ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Sekondari ya
Mbebe.
Mkuu wa Sekondari ya Nakalulu Ndg.Charles Mpelegwa iliyopo katika Kata
ya Isongole akipokea maelekezo kutoka kwa RC Mwangela wa Songwe kuhusu
kukamilisha ndani ya majuma mawili ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Andrea Kalinga Diwani wa Kata ya Mbebe akitoa sababu za kusuasua
kwa ujenzi wa madarasa katika sekondari ya Mbebe kwaajili Kidato cha
Kwanza 2020.
Mohamed Mwala Diwani wa Kata ya Itumba –Ileje aliyevaa shati jeupe
akiwa katika pozi la aina yake baada ya kutoa sababu za kutokamilisha
ujenzi wa chumba cha darasa.
Hapa ni Itumba Sekondari ambapo RC wa Songwe aliwataka viongozi wa
wilaya na kata kutozipa nafasi siasa zinazokwamisha maendeleo.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Songwe anayesimamia masuala ya elimu Ndg.Kornel Ntulo akitoa majumuisho ya ziara ya RC Mwangela aliyoifanya wilayani Ileje akifuatilia mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2020,hapa ilikuwa ni katika Ukumbi wa hoteli ya VIM Itumba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...