Shirikisho la soka barani Afrika wamemtaja mwanasoka bora wa mwaka kuwa ni Sadio Mane ambaye anachezea timu ya Liverpool.
Walioshiriki
kinyang'anyiro cha tuzo hizo ni mshambuliaji wa Senegal na klabu ya
Liverpool -na wenzie walioshiriki kinyang'anyiro hicho ni mchezaji wa
Misri Mohamed Salah na mchezaji wa Manchester City pamoja na winga wa
Algerian Riyad Mahrez.
Mane ambaye ana umbaye ana umri wa miaka
27, aliweza kuisaidia Reds katika ligi ya mwaka 2018-2019 na kufunga
magoli 30 katika msimu uliopita.
Aliweza kufunga magoli 15 mpaka sasa kwa mwaka 2019 mpaka 2020, na
kuisaidia Liverpool kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya
alama 13.
"Nina furaha sana na ninajivunia kuwa mshindi. Kandanda ni ajira yangu ambayo ninaipenda," alisema Mane."Ninapenda
kuwashukuru familia yangu, taifa langu , timu yangu ya taifa ,
wachezaji wenzangu, shirikisho na klabu ya Liverpool.Hii ni siku kubwa
kwangu."
Mane alichukua tuzo yake katika sherehe zilizofanyika huko Hurghada, Misri.Lakini si Salah, ambaye alishinda tuzo hiyo mara mbili katika miaka miwili iliyopita wala Mahrez wali.
Mane alimaliza katika nafasi tatu za juu katika tuzo hizo katika miaka mitatu iliyopita.Na ilikuwa ni ndoto yake kushinda tuzo hiyo ili kufikia mafanikio ya shujaa wake El Hadji Diouf, ambaye alishinda mwaka 2002.
kusoma zaidi bofya HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...