KAMATI ya Utendaji ya Chama cha  Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) , inawahimiza wanachama wake ambao wana nia ya kushiriki Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho kuhakikisha wanathibitisha kwa maandishi ili waweze kuhudhuria mkutano huo.

Hatua hiyo inatokana na mwitikio mdogo wa waliothibitisha kushiriki, hivyo kufanya maandalizi mengine ya mkutano huo kushindwa kufanyika vizuri. 
 
Kwa mazingira hayo mwisho ya kuthibitisha kushiriki itakuwa Jumatatu Januari 13 mwaka huu, na mkutano huo sasa utafanyika Jumapili Januari 19 na hakutakuwa na muda wa ziada kwa watakaoshindwa kuthibitisha.

 Lengo la mkutano huo  ni kujadili masuala mbalimbali ya chama, ambapo pia utapokea taarifa kutoka Kamati ya Marekebisho ya Katiba iliyoundwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na pia utapokea mapendekezo kutoka Kamati ya Utendaji ya TASWA  inayomaliza muda wake.

Watakaohudhuria Mkutano Mkuu Maalum ni wanachama wote walio katika leja baada ya kushiriki uchaguzi wowote wa TASWA kuanzia mwaka 2004, 2007, 2010, 2014 na wanachama wapya wote walioingia kuanzia mwaka 2015 hadi Juni mwaka jana.

Kwa mazingira hayo ili mkutano ufanyike kwa ufanisi ni vyema yeyote mwenye nia ya kushiriki athibitishe kwa maandishi akitaja jina lake na chombo na kutuma kwa email: taswatz@yahoo.com au mgosius@yahoo.com au machagift@gmail.com,   ili taratibu nyingine ziendele.
Nawasilisha,
 Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
  10/01/2020

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...