Pichani ni Ndg. Evarist Mrema Kaimu Mkuu wa Kanda ya Ziwa (TBS) akifafanua malengo ya Semina wakati walipokutana na washiriki wa semina Mkoani Geita.
Pichani wanaonekana Miongoni mwa washiriki katika semina ya mafunzo iliyoratibiwa na TBS wakiuliza maswali ya ufafanuzi juu ya Mambo ya Usajili na namna ya kupata alama ya Ubora.
Pichani ni Bi. Fatuma Namuniko Afisa Viwango kutoka TBS akizidi kuwapa madini washiriki wa semina juu ya umuhimu wa Viwango katika bidhaa na Biashara zao, katika Ukumbi wa JJ Hotel Mkoani Geita.
Pichani Ndg. Hamisi Sudi Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania akitoa ufafanuzi wa masuala ya Usajili wakati akizungumza na wanahabari Mkoani Geita.
Pichani ni Mhe. Josephat Maganga Mkuu wa Wilaya Geita akizungumza na washiriki wa semina ya mafunzo kutoka TBS (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo Mkoani Geita.
Na Abdullatif Yunus Michuzi TV
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wanaendelea na Semina ya Mafunzo kwa Wazalishaji, wasindikaji, wasambazaji, Watunzaji wa bidhaa, Chakula na Vipodozi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Semina yenye, malengo ya kutoa Elimu juu ya Viwango na Ubora Wa bidhaa ikiwa pamoja na kuelekeza utaratibu wa kufuata ili kupata leseni ya kutumia alama ya Ubora ya TBS ( TBS Quality mark license), wakiwa Tayari wamefika Mkoani Geita baada ya kumaliza Mkoani Kagera.
Akitoa Salaam zake za ufunguzi wa Semina hiyo Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga amewakumbusha washiriki wa semina hiyo juu ya faida za ushiriki wao katika mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa zao, kuuza bidhaa hizo nje ya maeneo yao, kuongeza Masoko, pamoja na kuwa na uhakika wa wateja kutokana na ubora wa Bidhaa kwavile tayari zitakuwa zimefuata utaratibu ikiwemo kuwa na alama ya ubora.
anasema Semina hiyo imebeba Elimu juu ya usajili wa majengo, bidhaa za vyakula na vipodozi, ambapo awali majukumu haya yalikuwa yakitekelezwa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), na sasa majukumu hayo yakiwemo na yale ya usajili majengo, maeneo ya kufanya biashara ya Chakula na Vipodozi yamerudishwa TBS hii ni kutokana na mabadiliko ya sheria ya fedha ya Mwezi Julai 2019
Katika semina hiyo washiriki wamefundishwa namna ya kuzifanya bidhaa zao kukidhi viwango kulingana na matakwa ya mlaji, ili kuifanya bidhaa hizo kukubalika katika viwango vya ndani na Nje ya Nchi kulingana na thamani ya Bei husika.
Sambamba na hilo pia washiriki hao wamendelea kufundishwa namna ya kujisajili Kwa njia ya mtandao wale wote wanaojihusiha na Majengo ya Biashara, Migahawa, maduka ya Vyakula pamoja na Vipodozi. Mafunzo hayo Mkoani Geita yamehudhuriwa na wafanyabiashara tofauti, katika Ukumbi wa JJ Hotel Katoro, na Sasa TBS wapo Mkoani Simiyu tayari kutoa Elimu kwa Umma na mafunzo kwa wafanyabiashara Wilayani Bariadi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...