Na Yassir Simba, Globu ya Jamii
TIMU ya taifa, Taifa Stars yaangukia kundi J katika hatua za awali kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia 2022 nchini Qatar.
Mashindano hayo yatakuwa na jumla ya makundi 10 ambayo yatacheza hatua awali kabla ya kupata timu 5 zitakazo wakilisha bara la Afrika katika fainali hizo za kombe la dunia.
Tanzania imeangukia kundi J sambamba na timu nyengine tatu ambazo ni Congo DRC, Benin na Madagascar.Mechi 120 za awali zinatarajiwa kupigwa kabla ya mechi 10 za mtoano ili kupata timu 5 ambazo zitawakilisha bara la Afrika katika kombe la Dunia mwaka 2022, nchini Qatar.
Makundi kundi A ni Algeria , Bukinafaso, Niger, Djibouti, kundi B ni Tunisia, Zambia, Mauritania na Guinea, kundi C ni Nigeria, Cape Verde, Central Afrika na Lieria, Kundi D ni Cameroon, Cote D' ivoire, Mozambiq na Malawi.
Kwa Upande wa Kundi E ni Mali, Uganda, Kenya na Rwanda.
Kundi linalotajwa kuwa ni kundi gumu zaidi ni kundi G lenye timu za Ghana,South Africa, Zimbabwe na Ethiopia.
Kundi F ni timu ya Egypt, Gabon, Libya na Angola, Kundi G ni Timu ya Ghana, Afrika Kusini, Zimbabwe na Ethiopia, Kundi H ni Senegar, Congo, Namibia na Togo, Kundi I ni timu ya Morroco, Guinea, Guinea-Bissau na Sudani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...