Mchunguzi wa Maaala wa vifaa tiba wa malaka ya Dawa na vifaa tiba, Saxon Mwambene akiwaonesha waandishi wa habari jinsi wanavyopima ubora wa Kondomu.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari na maafisa wa habari wa serikali pamoja na taasisi za serikali jijini Dar es Salaam leo wakati wa ziara ya kutembelea Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam leo.
Mchunguzi wa Maaala wa vifaa tiba wa malaka ya Dawa na vifaa tiba, Saxon Mwambene akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea maabala ya Dawa na vifaa tiba jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja ya maafisa mawasiliano wa serikali na taasisi za serikali kwa upande wa Afya.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
BIDHAA za chakula na dawa na vipodozi za kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 22 ziliteketezwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 ambavyo ni sawa na tani 140,705.25 ambapo kiwango hicho kilipungua mwaka 2018/2019 na kuteketeza tani 664.68
Kulingana na hilo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeweza kupunguza bidhaa zisizokidhi vigezo kwa kiwango kikubwa katika soko la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya maafisa mawasiliano wa serikali na taasisi za serikali pamoja na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Adam Fimbo jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba imefuatilia kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha bidhaa zisizokidhi vigezo zisitumiwe na walaji.
Hata hivyo TMDA katika kufuatilia ubora wa bidaa za chakula na dawa na vipodozi sampuli 1,136 za dawa za bianadamu zilichunguzwa kwa kipindi cha miaka minne ambapo ni sawa na asilimia 96 zilikidhi vigezo vya ubora ikiwa asilimia 90 ya sampuli 144 za dawa za mifugo nazo zilikidhi vigezo.
Aidha TMDA imeidhinisha dawa za majaribio 189yanayofanyika hapa nchini yanazingatia sheria, kanuni, miongozo na vigezo vya kitaifa na kimataifa katika majaribio hayo.
Kwa upande wa kudhibiti madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi TMDA imeweka mifumo mifumo madhubuti ya kuweza kutambua, kutathmini na kuzuia madhara yasiyovumilika yasitokee kwa wananchi.
Fimbo ameeleza kuwa TMDA kwa kipindi cha miaka minne wameweza kusajili maeneo 32,860 za biashara za bidhaa zilizodhibitiwa ikiwa ni pamoja na maghala ya kuhifadhi bidhaa maeneo ya usambazaji, maduka ya jumla na rejareja ya bidhaa.
Hata hivyo fimbo ameeleza kuwa TMDA wameweza kutoa msaada wa kiufundi kwa viwanda na uanzishwaji wa viwanda vipya 12.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...