Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo akiongea na Wakazi wa Arusha wakati wa Uzinduzi wa kampeni za
kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya
Mkoani Arusha, ambapo aliwataka watanzania kujiunga na mpango huu na
kuwapuuza wanaoposha kuhusu vifurushi kwani hawana nia njema na afya za
watanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiongea na Wakazi
wa Arusha wakati wa Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga
na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani Arusha, ambapo alisema
aliwataka watanzania iwapo akifanya kazi matumizi ya kwanza iwe afya
yako, na kuwataka kutoweka rehani maisha yao, kwani hautaweza kuwa na
maendeleo kama hauna uhakika wa huduma za matibabu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo akitoa kadi za bima ya afya kwa baadhi ya wakazi wa Arusha
waliojiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya, wakati wa Uzinduzi
wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Vifurushi vya
Bima ya Afya Mkoani humo
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya Bernard Konga Wakazi wa Arusha wakati wa Uzinduzi
wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Vifurushi vya
Bima ya Afya Mkoani Arusha, ambapo alisema ifikapo 2025 NHIF inataka
zaidi asilimia 75 ya watanzania wawe wamejumuishwa katika mfumo wa bima
ya afya.
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
………………….
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho
Gambo amesema kuwa wanaopinga utaratibu wa vifurushi vya bima ya afya
hawawatakii mema watanzania.
Hayo ameyasema leo wakati
akizindua mpango wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na NHIF kupitia
vifurushi vipya katika soko la Mbauda jijini Arusha.
“Ukisikia mtu anapinga mpango
huu hakutakii mema kwani pindi unapopatwa na matatizo hatakuja
kukusaidia hivyo tuwapuuze na tujiunge na mapango huu wa bima ya afya,”
alisema Mhe. Gambo.“Gharama za matibabu kwasasa
ni kubwa sana, unaweza kwenda hospotali gharama za matibabu zikawa ni
kubwa kuliko kifurushi cha bima ya afya, ndugu zangu tujiunge na mpango
huu ili tuwe na uhakika wa matibabu wakati wowote”-Alisisitiza Mhe.
Gambo.
Kutokana na umuhimu huo
amewataka viongozi wa mkoa pamoja na viongozi wa dini kushirikiana kwa
pamoja katika kuwahimiza na kuwakumbusha wananchi juu ya kuwa na bima ya
afya.
Alisema mpango wa vifurushi vya bima ya afya unamwezesha mwananchi kupata tiba popote pale nchini bila ya usumbufu wowote.“Bima ya Afya chini ya
uenyekiti wa Mhe. Mama Anne Makinda imekuwa ni bima ya afya iliyoimara
sana, nakupongeza sana kwa kazi kubwa uliyoifanya wewe na bodi yako,”
alisema.
Alisema kuwa pamoja na
Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha Mfumo wa Bima ya Afya pia imeendele
kuboresha miundombinu ya maeneo ya kutolea huduma ili mwananchi
anapokuwa na kadi yake ya bima anakuwa na uhakika wa matibabu na yenye
kiwango bora.
“Mimi ni balozi mkubwa sana wa
mpango huu wa bima ya afya kwasababu najua umuhimu wake hasa wakati mtu
anapopatwa na maradhi, unapokuwa na kadi unakuwa na amani ndani ya
familia yako wakati wote,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya
NHIF, Mama Anne Makinda amesisitiza wananchi juu kuweka kipaumbele
katika suala zima la bima ya Afya ndani ya familia zao.
“Ukifanya kazi matumizi ya
kwanza iwe afya yako, tusiweke rehani maisha yetu, hautaweza kuwa na
maendeleo kama hauna uhakika wa huduma za matibabu,” alisema Mama
Makinda.Alisema kuwa kadi ya vifurushi inamuwezesha mwanachama kupata huduma za matibabu popote anapokuwa ndani ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...