Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa
 Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu  ameagiza kukamatwa mara moja kwa 
Wazazi wanaowazuia ama kutokuwapeleka Watoto wao shule wale ambao 
wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza.
Gavana
 Shilatu ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi wa shule ya 
Sekondari ya Mweminaki iliyopo kata ya Kitama wakati wa ziara yake ya 
kutembelea shule zote za Sekondari zilizopo Tarafa ya Mihambwe ambapo 
hakuridhishwa na kiwango cha kuripoti shuleni kwa Wanafunzi waliofaulu 
kidato cha kwanza.
"Nazungumza
 nanyi Wanafunzi ambao mnawajua Wanafunzi wenzenu waliofaulu kidato cha 
kwanza na wapo nyumbani. Nendeni mkawaambie Wazazi wao watakaokaidi 
kuwapeleka shuleni Watoto wao Serikali itatumia vyombo vyake kuwakamata 
wote. Usalama wao wawalete Watoto shule mara moja." Alisema Gavana 
Shilatu
Akizungumza na 
Mwandishi wetu mara baada ya ziara hiyo Gavana Shilatu alisema sababu 
wanazotoa Wazazi za kushindwa kuwapeleka Watoto shule hazina mashiko ni 
za kuishi kwa mazoea kutokana na mwamko mdogo uliopo licha ya Serikali 
kutoa Elimu bure.
"Mwaka 
jana walisema hawana hela hata ya kununua sare za shule kutokana na 
malipo ya Korosho kuchelewa, mwaka huu wamelipwa fedha za Korosho kwa 
wakati lakini bado hawawapeleki Watoto shule, hapa tatizo si fedha. Sasa
 mwendo ni ule ule tutawakamata wote wasiowaleta Watoto shule." 
Alisisita Gavana Shilatu.


 

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...