NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
WAZIRI wa TAMISEMI ,Suleimani Jafo, amemuelekeza kaimu mkurugenzi wa shirika la elimu Kibaha,Robert Shillingi ,kusimamia shirika hilo na kuandaa timu ,ili kuwadhibiti baadhi ya wataalamu na watendaji ambao wanajigeuza miungu watu kwa kukandamiza watumishi wa chini .
Aidha amekemea tabia ya baadhi ya maofisa utumishi wanaoandaa miongozo ya roho mbaya na kukwamisha taarifa za watumishi waliojiendeleza.
Akizungumza wakati wa kusheherekea maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa shirika la elimu Kibaha,Jafo alisema kuadhimisha kwa
miaka hiyo ni vyema wakatathmini shirika lilipo toka na lilipo ili
kujirekebisha changamoto zilizopo.
"Menejimenti mnakazi
ya acheni tabia ta umimi, ndio jambo kubwa la kulifanya ,wakati
mnaadhimisha miaka 50 inapaswa kujitathmini na kuona wapi mlikosea ili
shirika lisonge mbele".
"Endeleeni kusimamia mambo
kwakuwa mlipotokea sipo tulipo ,nawapongeza sana mlipofikia ila
endeleeni kusimamia machache yaliyobaki"alisema Jafo .
Hata hivyo Jafo alieleza , halihitajiki kuwa shirika ombaomba na
anatamani liendelee kukua kiuchumi. "Tulipita katika kipindi kigumu
hususan ya mikataba ya uwekezaji iliyokuwa hailingani na thamani ya
mali"
Alifafanua adui ya wataalamu ni wataalamu wenyewe, kuna wataalamu wengine kazi yao kutoa miongozo ya roho mbaya .
"Kizazi
cha shirika la elimu kuweni na upendo ,msikandamizane kwenye majukumu
yenu ,kwakuwa tunapata taarifa za malalamiko kutoka kwa watumishi wa
chini na wengine wanadai wanateswa."
Kuhusu changamoto
ya miundombinu alieleza,serikali tayari imeshatoa Trilioni moja kwa
ajili ya elimu bila malipo, na pia kutokana na hali ya shule ya
sekondari ya Kibaha kuwa mbaya ilitolewa sh. bilioni moja fedha
iliwekezwa kwa kuboresha miundombinu hiyo.
Akitolea ufafanuzi, kero ya usafiri usio wa uhakika ambapo kuna kero ya magari ya abiria hayapiti Tumbi na kusababisha wagonjwa kupata shida ya kutoa gharama za pikipiki au tax alimuelekeza mkuu wa mkoa wa Pwani, kushughulikia suala hilo.
Nae kaimu mkurugenzi wa shirika hilo, Robert Shillingi alitaja ,changamoto ufinyu wa bajeti na uchakavu wa miundombinu .
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuna malalamiko kuhusu changamoto za kiutendaji katika hospital ya Tumbi wa baadhi ya watumishi na kuomba wajirekebishe na badala yake watoe huduma bora.
Ndikilo alieleza kutokana na tatizo la bajeti ni vyema wakatumia ardhi iliyopo chini yao kuiendeleza ili kujiongezea kipato ,hivyo alimuomba Jafo kutilia msukumo kupata kibali serikalini,TAMISEMI cha andiko lililoandikwa ili waendeleze ardhi iliyopo kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...