WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo ihakikishe asilimia
tatu ya wakulima wa zao la korosho waliosalia wanahakikiwa na kulipwa.
Hadi sasa zaidi ya asilimia 96 ya wakulima wa korosho waliouza korosho zao katika msimu wa 2018/2019 wameshahakikiwa na kulipwa.
Ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Januari 3, 2020) wakati alipokutana na baadhi ya
wakulima wa korosho kutoka wilaya za Ruangwa, Masasi na Tandahimba.
Baada
ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima hao, Waziri Mkuu amewataka
waendelee kuwa na subira na kwamba haki yao itapatikana.
“Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ipo
makini, hivyo hakuna Mtanzania yeyote atakayepoteza haki yake.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa wanachama wa vyama vya ushirika pale
watakapoona ushirika wao hauendi vizuri wasisite kutoa taarifa
Serikalini.
Amewaagiza
wakuu wa mikoa na wilaya wawachukulie hatua viongozi wote wa vyama vya
ushirika watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Kwa upande wao, wakulima wameishukuru Serikali kwa kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi na kwamba wanaimani ya kulipwa madai yao.
Mmoja
wa wakulima hao Bi. Mariamu Mganda amesema anamshukuru Waziri Mkuu kwa
kukubali kuwasikiliza kwani wamepata tumaini la kulipwa fedha zao.
Mkulima
Mwingine Bw. Abdulkareem Said amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa
Serikali hususan baada ya Waziri Mkuu kukubali kusikiliza kero zao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo, Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Lindi na Mtwara, Makatibu Tawala
wa Mikoa hiyo, Wakurugenzi wa Benki ya TADB na CPB, katika Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, kabla ya kikao na Wakulima wa
zao la korosho wa Mikoa hiyo, Januari 3, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Wakulima wa zao la korosho wa
Mkoa wa Mtwara na Lindi, katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,
Januari 3, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...