Na Sultani Kipingo wa Michuzi TV
WAZIRI Mkuu mpya wa Finland Sanna Marin amependekeza nchi hiyo iwe na siku nne tu za kufanya kazi ili wananchi wawe na fursa kuwa na familia zao kwa muda mrefu Zaidi na kufanya mambo mengine ya jamii ikiwemo michezo na utamaduni. 
 Marin, akiwa kiongozi mkuu wa serikali mdogo kuliko wote duniani kwa kuongoza nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 34, amependekeza pia kwamba muda wa kazi uwe saa nne badala ya nane kwa siku. 

Kiongozi huyo mwenye mtoto mmoja anaongoza muungano wa vyama vya mlengo wa kati-na-kushoto akiwa na viongozi wengine wa vyama vinne ambavyo vitatu vinaongozwa na wadada wenye umri wa chini ya miaka 35. 

 Katika mahojiano alisem: “Naamini wananchi wana haki ya kutumia muda wao mwingi na familia zao, wapenzi wao na mambo mengine katika Maisha kama vile hobby na utamaduni. Hii itakuwa hatua kubwa kwetu katika Maisha ya kazi”. 

Kabla ya kuwa Waziri Mkuu Marin alikuwa Waziri wa Uchukuzi wa Finland, ambapo hata huko wizarani alipigania swala la kuwa na siku chache za kufanya kazi katika wiki ili kuongeza ufanisi na tija. 

 Hivi sasa nchini Finland kufanya kazi saa nane kwa siku na siku tano kwa wiki ni jambo la kawaida. Pendekezo hilo limeungwa mkono mara moja na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Bi. Li Andersson, ambaye ni kiongozi wa chama cha Left Alliance. 
Bi. Andersson alisema: “Ni jambo la mihumu kuruhusu raia wa Ufini kufanya kazi kwa kiasi. Hili sio swala la kutawala kwa staili ya kijinsia bali pia ni kusaidia na kutekeleza ahadi kwa wapiga kura”. 

Katika nchi jirani ya Sweden, ambako mfumo wa kufanya kazi kwa siku sita kwa wiki ulijaribiwa mwaka 2015, matokeo yalionesha kwamba wafanyakazi wamekuwa wenye furaha Zaidi, matajiri na wenye kuleta tija. 
Mapema mwezi Desemba mwaka jana baraza la chama tawala cha nchio hiyo Social Democratic Party kilipitisha kwa kura 32-29 jina la Sanna Marin dhidi ya Antti Lindtman kuchukua kiti cha uwaziri mkuu kutoka kwa aliyekuwa anashika nafasi hiyo Antti Rinne. 
 Na mnamo Mwezi November mwaka jana kampuni ya Microsoft Japan ilifanya uamuzi mgumu wa kuboresha Maisha ya kazi kwa kuanzisha weekend ya siku tatu kwa wafanyakazi wake. Matokeo yalionesha tija kupanda kwa asilimia 39.9!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...