Daktari Hamadi Khamis Makame
akimtoa damu Mtoto Huda Abdalla Abdillahi mkaazi wa Kikwajuni katika
Zoezi la utoaji wa Damu kwa ajili ya kupima Malaria yaliogundulika zaidi
katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50 wamegundulika Kikwajuni
Majumba ya Mjarumani Zanzibar.

Daktari Hamadi Khamis Makame
akimtoa damu Mtoto Omari Mjaka Idarous mkaazi wa Kikwajuni katika Zoezi
la utoaji wa Damu kwa ajili ya kupima Malaria yaliogundulika zaidi
katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50 wamegundulika Kikwajuni
Majumba ya Mjarumani Zanzibar.

Wananchi mbalimbali waliohudhuria
katika Zoezi la utoaji wa Damu kwa ajili ya kupima Malaria
yaliogundulika zaidi katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50
wamegundulika Kikwajuni Majumba ya Mjarumani Zanzibar.

Meneja Mratibu wa Malaria Unguja
na Pemba Abdalla Suleiman akiwa pamoja na Naibu Meneja Faiza Abbas
wakishajiisha watu kwenda kutoa Damu kwa ajili ya kupima Malaria
yaliogundulika zaidi katika Shehia hio ambapo kiasi cha watu 50
wamegundulika Kikwajuni Majumba ya Mjarumani Zanzibar.
……………….
Na Khadija Khamis ,Maelezo Zanzibar
Meneja Mratibu wa
Malaria Zanzibar Abdalla Sleiman Ali ameitaka jamii kuweka tahadhari
kutokana na ongezeka la wagonjwa wengi ambao wamegundulika na vimalea
vya malaria nchini.
Akizungumza
katika zoezi la upimaji wa malaria katika kaya mbali mbali za Shehiya ya
Kikwajuni Juu amesema takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia mwezi wa
oktobar, novembar na disemba, jumla ya wagonjwa 33 wamelazwa katika
hospitali kuu ya Mnazimmoja na wagonjwa 4 wamefariki dunia.
Amesema kuwa
maeneo yamegundulika uwepo wa watu wenye ugonjwa huo katika miezi minne
waliweza kuwatibu wagonjwa 50 kutoka kikwajuni bondeni wagonjwa 17
kikwajuni juu wagonjwa wengine katika shehiya mbali mbali ikiwemo
Miembeni, Kwahani, kwaboko ,wilaya ya kati kaskazini A na B maeneo yote
hayo yamegunduliwa kuna wagonjwa wa malaria .
aidha
amewasisitiza wananchi kutumia ipasavyo vyandarua pamoja na kusafisha
mazingira yaliyowazunguka ili kuepusha mbu kuzaliana na kusababisha
kuzidi kuongezeka kwa ugonjwa huyo nchini.
Alifahamisha
zoezi la upimaji damu wa wananchi kutasaidia kugundua mapema wananchi
ambao wanamaambukizo ya malaria na kupatiwa matibabu kwa haraka jambo
ambalo litasaidia kuenea kwa maambukizo ya maradhi hayo.
Akieleza sababu
za kuenea kwa haraka maradhi hayo alisema kuwa hii inachangia kutokana
na utumiaji mdogo wa vyandarua katika jamii .watu kutoka nje ya Zanzibar
pia husababisha kuigiza maradhi hayo pamoja mabadiliko ya hali ya hewa
joto na mvua husababisha unyevu unyevu na kutuwama maji kuwa mazalio
ya mbu .
Hata hivyo
alifahamisha baadhi ya wavuvi waliopimwa ambao wanaotokea katika maeneo
hayo kati ya wavuvi 29,waliopimwa 19 wamegundulika na vimalea hivyo .
Akitoa wito kwa
jamii mtu akijigundua na ishara na dalili afike haraka katika vituo vya
afya kwa kupatiwa matibabu asikae nyumbani ,kukaa nyumbani
kutahatarisha maisha yake.
Nae Daktari
kutoka Timu ya Malaria kwa Wilaya ya Mjini Hamad Khamis Ali amesema
tokea kuanza kwa zoezi hilo jumla ya watu watano wameshagundulika kuwa
na vimelea vya ugonjwa wa malaria.
zoezi hilo
litafanyika kwa siku mbili kwa kila haya katika maene ya kikwajuni juu
na kikwajuni bondeni kutokana na kuzuka kwa wagonjwa wengi katika eneo
hilo pamoja na kuonekana kumekuwa na mazingira hatarishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...