Charles James, Michuzi TV
WATUMISHI wa Mahakama nchini wametakiwa kufuata sheria na kanuni zilizopo pindi wanapofanya maamuzi ili wananchi waendelee kuwa na imani na chombo hicho cha kimaamuzi.
Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Augustino Mahiga wakati alipokua akizindua mwongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili ya maafisa wa mahakama.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Dk Mahiga amesema kwa muda mrefu watanzania wamekua wakiamini chombo pekee kinachoweza kutenda haki ni mahakama hivyo watumishi wake wana kila sababu ya kutunza imani hiyo ya wananchi.
Amewaonya watumishi wachache wanaokiuka maadili ya Mahakama kuacha mara moja tabia hiyo ili kulinda heshima ya Mahakama na kulinda ajira zao kwani serikali ya awamu ya tano haipo tayari kuona inachafuliwa na mtu yeyote.
" Kwa mujibu wa Ibara ya 107 ya Katiba yetuni Mahakama pekee ndio yenye jukumu pekee la kutoa haki, hivyo ni wito wangu kwa watumishi wa Mahakama zetu kuendelea kutunza imani hii.
Ninaamini kwa kuzingatia muongozo huu kutaondoa ile migongano ama malalamiko yanayokua yakitolewa na kamati za maadili hayatakuepo tena kwani kila mmoja atajua majukumu na mipaka yake," Amesema Dk Mahiga.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imekua na kipaumbele cha kuimarisha maadili kwa watumishi wa umma ili kuongeza imani ya wananchi kwa serikali yao jambo ambalo anaamini limekua na mafanikio makubwa.
" Ni wazi sasa wananchi wanaridhishwa na maadiili ya watumishi wetu wa umma hasa katika utoaji wa huduma zinazotolewa kwenye maeneo na sekta mbalimbali wanazoenda kupatiwa huduma," Amesema Waziri Mahiga.
Pia ametoa wito kwa Wizara ya TAMISEMI kutoa ushirikiano wa kibajeti kwa kamati za maadili za Mahakama za Wilaya na Mikoa pindi wanapohitajika kufanya hivyo.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ndio wenyeviti wa kamati za maadili kwenye maeneo yao kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kukuza maadili nchini.
Ameahidi pia kuhakikisha Tume ya Utumishi inatoa elimu ya kisheria kwa wananchi kwani asilimia kubwa ya watanzania wamekua hawana uelewa mpaka wa mambo ya kisheria jambo linalosababisha muda mwingine kuona mahakama hazitendi haki tu kwa sababu ya kutokua na uelewa.
Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wenzake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe Rehema Nchimbi amesema wataendelea kupigania umuhimu wa maadili kwa watumishi wa umma na kamwe hawatakubali kuona mtumishi yoyote akichafua serikali kwa kukosa maadili.
Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Dk Augustino Mahiga (katikati) akizindua mwongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili ya maafisa wa mahakama. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dodoma na kuhudhuria na Jaji Mkuu, Prof Ibrahim Juma ( wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege (wa pili kulia).
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustino Mahiga (wa pili kushoto waliokaa), Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma (wa katikati) na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe Josephat Kandege (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa mahakama leo jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mahakama wakiongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Dk Augustino Mahiga na Jaji Mkuu, Prof Ibrahim Juma wakiwa na vitabu vya mwongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili za maafisa wa mahakama katika uzinduzi wa miongozo hiyo leo jijini Dodoma.
Waziri
wa Sheria na Katiba, Balozi Dk Augustino Mahiga akizungumza katika
hafla hiyo ya Uzinduzi wa mwongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili ya
maafisa wa mahakama jijini Dodoma.
Watumishi
wa mahakama kutoka Kanda mbalimbali nchini ambao wamehudhuria kwenye
hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili za
maafisa wa mahakama uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa wenzake na Wakuu wa Wilaya kwenye uzinduzi huo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma akizungumza na watumishi wa mahakama katika hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili ya maafisa wa mahakama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...