Tanzania imetajwa kuwa kuwa ngome ya Amani Barani Afrika kwa kuwafanya raia wake na taifa kwa ujumla kuishi kwa amani na kuendelea kutoa misaada ya Ulinzi wa Usalama katika nchi jirani zinazokumbwa na machafuko ya kisiasa.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Balozi mteule wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Regina Hess wakati wa hafla ya uzinduzi wa karakana kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyojengwa na Serikali ya Ujerumani kwa gharama ya Tsh. Bilioni 8.5.

Alisema mafanikio hayo yote hayawezi kuja bila kujitoa na kugharimu muda na kusabisha baadhi ya hao walioleta mafanikio kupoteza maisha katika oparesheni mbalimbali za kijeshi na muhimu kuwakumbuka hao mashujaa na kuwakumbuka familia na ndugu zao.

“Tanzania imefanikiwa kushiriki katika oparesheni mbalimbali kama ile ya Moniscu (Boma), UN ARMIT (Dafuu), na Afrika ya Kati (minuska) na pia Lebanoni, kwa kufanya hivyo Tanzania imekuwa ngome ya ulinzi wa amani na usalama katika ukanda wa Afrika” alisema Balozi Hess.

Sambamba na hilo Balozi Hess alibainisha, mbali na ushirikiano wa kijeshi wanao shirikiana na Tanzania, bado wanaendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania hususani Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika upande wa afya kwa kujenga hospitali na baadhi ya miundombinu ya kijeshi.

“Ujerumani tunajikita kwenye masuala ya usafirishaji na maswala ya afya na hii karakana moja mpya ni mfano mmoja katika masuala ya usafirishaji na katika afya ni vituo vya afya vinavyohamishika vilivyofika 2019 vitachangia sana kupambana dhiti ya virusi vya Corona” alisema Balozi Hess.

Aidha Balozi Hess aliwahakikishia Watanzania kuwa juhudi za Ujerumani hazitaisha katika kuiunga mkono JWTZ, na badala yake itaongeza mikakati na malengo ya ya kuisaidia Tanzania ikiwemo kuweka programu mpya endelevu ya kuisaidia Tanzania katika maeneo mengi ambayo tayari imeshaidhinishwa.

Karakana hiyo ya jeshi la JWTZ kikosi namba 501 imefadhiliwa kupitia ushirikiano wa Umoja wa Tanzania na Ujerumani wenye gharama za bilioni 8.5 uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana kwa kugonganisha miguu na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Regine Hess baada ya sherehe za uzinduzi wa Karakana Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 13, 2020.  Picha na IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...