Benki ya CRDB imezindua mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja
kwa njia ya QR Code.
Akizindua mpango huo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Tully Esther Mwambapa alisema, Njia hiyo itamwezesha mteja kutoa maoni kwa Benki bila usumbufu wowote
na kwa muda mfupi sana.
"Anachotakiwa kufanya mteja ni kuscan kwenye QR
Code kwa kutumia simu yake ya smart ambayo imeunganishwa na internet, Mteja atafungua camera ya simu yake na kuscan kwenye QR Code ambazo
zinapatikana kwenye matawi yote ya Benki halafu itampeleka moja kwa mojo
kwenye website ya CRDB Bank, huko atakutana na maswali ambayo
yatamwongoza kwenye kutoa maoni; ikiwa, kuona listi ya Matawi yote ya
Banki ambayo atatakiwa kuchagua tawi ambalo anahitaji kulitolea maoni na
baada ya hapo atatuma amoni yake, Maoni hayo yatakwenda moja kwa moja
kwenye kitengo husika cha Benki ya CRDB na kufanyiwa kazi".
Aidha
Mkurugenzi wa Mawasiliano amewataka wateja kutumia huduma hii
kuwasilisha maoni yao amboyo kwanamna moja yatasaidia kuboresha
huduma za kibenki na kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa weledi
mkubwa zaidi bila wasiwasi.
Uzinduzi wa mpango huo wa kutoa maoni, umeanza kutimiwa na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye
huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo
nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (katikati) akinguzumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati
wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB,
Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushoto ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, George Yatera.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akionyesha namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushuhudiwa na wafanyakazi wengine wa Benki hiyo. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa
(wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki
ya CRDB, Yolanda Urio (kulia) wakimuelekeza mmoja wa wateja wa Benki ya
CRDB, namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha
maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo
uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es
salaam, leo Machi 17, 2020. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na
Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo
itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Matawi wa Benki ya CRDB, Bonventura Paul
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio (kulia) wakimuelekeza mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, Beatrice Bariki namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es salaam wakionyesha namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...