Benki ya CRDB imezindua mpango maalum wa kuwawezesha wafanyakazi wanawake katika nyanja mbalimbali ili waweze kushika nafasi za uongozi.
Akizindua mpango huo katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,
Abdulmajid Nsekela alisema, Mpango huo ni mahususi katika kuwawezesha
wanawake wa CRDB Banki ili waweze kuwa viongozi katika nyanja mbalimbali pamoja na kuwafanya waweze kujiamini na kukamata fursa zilizopo.
Mpago huo ni mwendelezo wa maadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani,
ambapo Benki ya CRDB imeamua kuadhimisha kwa kuzindua program
maalum na kuwapa semina wanawake wa Benki ya hiyo.
Aidha Nsekela alisema mpango huo utakuwa endelevu kwani Benki ya CRDB
sio tu kuwa inaamini katika nafasi sawa yaani 50/50, bali imeona ni vema
kuwa na mpango maalumu kwa kuwafanya wanawake wawe
na wigo mpana zaidi kuweza kupambana kwa kujiamini na kushika nafasi na
nyazifa mbalimbali za uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akiwakiwaonyesha wakurugenzi wengine wa Benki hiyo, moja ya tuzo zenye jumbe mbalimbali, wakati wa uzinduzi wa program maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women) ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa program maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women) ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.
Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza na
baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa program
maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women)
ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye
ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kulia) akizungumza wakati wa mdahalo ulioenda sambamba na uzinduzi wa program
maalumu ya kuwawezesha Wanawake (Mentoring Program for empowering Women)
ili waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi, iliyofanyika kwenye
ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...