Benki ya Exim Tanzania hii leo imetangaza washindi watano wa mwezi katika kampeni yake ya 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard'. Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwatangaza washindi wa droo ya kwanza wa kampeni hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja benki ya Exim Bwana Frank Matoro aliwataja washindi hao kuwa ni pamoja Fahim Mohamed ( Dar es Salaam), Baraka Rom Kimaro (Dar es Salaam), Hendrick Hopley (Arusha), Humphrey Henry ( Mbeya) na Amani Makungu (Zanzibar) ambao kila mmoja atazawadia simu janja (smartphone).
"Ifahamike kwamba mpaka sasa wateja 40 wameshajishindia vocha za manunuzi zenye thamani ya sh 50,000 kila mmoja na zinaendelea kutolewa kila wiki.Pia tunatoa zawadi kama hizi za leo za simu janja kwa washindi watano kila mwezi hadi mwisho wa mwezi Aprili, 2020 kwani ndio tutakuwa tunafika kilele cha kampeni yetu’’
‘’Katika kuhitimisha kampeni hii tutatoa zawadi kubwa zaidi kwa washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza ataenda Dubai, mshindi wa pili ataenda Cape Town, Afrika Kusini na wa tatu ataenda visiwa vya Zanzibar. Washindi hao pamoja na wenza wao watagharamiwa gharama zote ikiwemo Visa, Tiketi ya Ndege pamoja na pesa za matumizi.'' alifafanua
Kwa mujibu wa Bw. Matoro, Kampeni hiyo inayoendelea ikishirikiana na Mastercard imeanza katikati ya mwezi Februari, 2020 ipo wazi kwa wateja wote wanaomiliki kadi za Exim Bank MasterCard, pamoja na wateja wote ambao wameomba au wataomba kadi mpya katika kipindi cha kampeni.
''Wanachotakiwa wateja wetu ni kufanya miamala yao kupitia kadi ya Exim Bank MasterCard mara nyingi iwezekanavyo kwa kuwa kila muamala unaongeza nafasi moja ya kushinda.''
''Habari njema ni kwamba wateja wanaotumia kadi zetu wamekuwa wakifurahia urahisi wanapofanya manunuzi au malipo ya mahitaji yao kwenye maduka tofauti tofauti(Shopping), ununuzi wa bidhaa kupitia mtandaoni, malipo wakati wa safari, malipo ya hoteli na shughuli za kitalii.'' alisema.
Maofisa waandamizi kutoka Benki ya Exim Tanzania akiwemo Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro (Kushoto) wakionyesha mbele ya waandishi kadi za Mastercard zinazotumiwa na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya kuwatangaza washindi washindi watano wa mwezi waliojishindia simu janja (smartphone) katika kampeni ya 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard' inayolenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi hizo katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya Exim Bi Mariam Mwapinga (Kulia) pamoja Afisa Bidhaa za Rejareja wa benki hiyo Bw Callist Butinga.
Meneja Masoko wa Benki ya Exim Bi Mariam Mwapinga (katikati) akizungumza na waandishi Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuwatangaza washindi washindi watano wa mwezi waliojishindia simu janja (smartphone) katika kampeni ya 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard' inayolenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi za Mastercard za benki hiyo katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro (Kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Muazo ya Kidigitali Bw Paritosh Babla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...