WAFANYABIASHARA na wakulima wa Mkoa wa Mtwara wametakiwa kutumia fursa za kilimo cha Korosho, Mihogo na Ufuta pamoja na mifugo ili ziweze kuwainua kiuchumi kupitia benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Benki hiyo imeendelea na mkakati wake wa kuzindua NBC Biashara Club katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania,ambapo hadi sasa wamezindua klabu iyo katika maeneo kumi na mbili, na leo imezindua NBC Biashara Club katika mkoa wa Mtwara.
Mgeni Rasmi wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) Mtwara, Said Swallah amesema katika NBC Biashara Club kuna fursa mbali mbali ikiwepo kuuza bidhaa nje ya nchi, na jinsi ya kutumia biashara za mpakani zinazojulikana kama Cross Border Trade.
Aidha, Swallah amesema kuna changamoto ya taarifa kutowafikia watu na imekuwa ni kikwazo, na kupitia forum ya namna hii ameona dhahiri wengi wanaweza kutumia nafasi hiyo kuingia na kufanya biashara izo na hatimaye kuingiza kipato na kukuza uchumi wa mkoa wa Mtwara.
“Tulianza biashara na watu wa Comoro katika kipindi kifupi sana na TCCIA wamekua wakiratibu mawasaliano ya kibiashara kati ya Comoro na Mtwara, lakini wapo ambao walianza kufanya biashara baada ya meli kufika. Baadae meli zilianza kupungua baada ya muamko kupungua katika fursa hiyo. Ni matumaini yangu kwamba kwa kupitia NBC Biashara Club, fursa kama izi hazitatupita tena.” amesema Swallah.
Akiongea katika hafla hiyo, Kaimu Afisa Biashara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Amani Lusaki ameipongeza Benki ya NBC kwa kuja na wazo zuri la Biashara Club ambapo imewakusanya wafanyabiashara mbali mbali na kuwahamasisha, kuwaelimisha na kuwafahamisha kuhusu fursa mbali mbali za biashara.
Aidha ametaja kilimo cha Korosho, Mihogo na Ufuta kua ni moja wapo ya fursa za mkoa huo na kwa upande wa mifugo kunayo fursa kubwa ya nyama na maziwa na kuwataka NBC kuwaunga mkono wafanya biashara wa Mkoa wa Mtwara kuzichangamkia fursa hizi ili waweza kuinua uchumi wa mkoa huo.
Naye Meneja wa bidhaa na huduma za kifedha NBC Makao makuu Dar es salaam, Jonathan Wilson Bitababaje amemalizia kwa kusema, wamezindua NBC club kwa lengo kubwa la kuwaleta wateja wao pamoja ili waweze kuungana katika eneo la biashara na pia kuwapa mafunzo.
Bitababaje amesema, mafunzo kwa wafanyabiashara hao ni kupata elimu kubwa sana ya kuzikuza biashara zao, na waweze kuendesha biashara zao katika hali ya ushindani na soko la nje ya nchi. “Tunawapa mafunzo ya ndan ni pia tunawapa mfiduo ya kwapeleka nje nchi kukutana na wafanya biashara wakubwa na wenye viwanda vikubwa iliwaweze kua wanaagiza bidhaa na kupata moja kwa moja kutoka viwandani.”
Klabu ya Biashara ya NBC hutumiwa kama sehemu ya utunzaji wa biashara na mkakati wa uaminifu wa wateja. Kusudi kuu ni utoaji wa huduma za msaada zisizo za kifedha kupitia mafunzo ya ustadi wa biashara na kuwajengea uwezo kwa wateja wa biashara wa NBC, kama sehemu ya safari yetu katika kuwaunga mkono.
Mmoja kati ya waliohudhuria kutoka TCCIA, Juma Napinda akitoa mada wakati wa tukio la uzinduzi wa NBC Business Club mkoa wa mtwara. NBC Business Club kwa sasa imeenea katika mikoa mbali mbali nchini ikiwemo Singida, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Njombe, Mbeya, Tanga pamoja na Lindi ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha, kuwaongezea ujuzi na kuwakuzia mtandao wafanyabiashara.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) Mtwara, Saidi Swallah (Kulia) akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa NBC Business Club mkoa wa Mtwara. NBC Business Club kwa sasa imeenea katika mikoa mbali mbali nchini ikiwemo Singida, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Njombe, Mbeya, Tanga pamoja na Lindi ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha, kuwaongezea ujuzi na kuwakuzia mtandao wafanyabiashara. Wengine pichani ni Meneja wa benki ya NBC tawi la Lindi, Nd Iovin Mapunda(kushoto) pamoja na Meneja wa benki ya NBC tawi la Mtwara, Nd. Emmanuel Mseti(katikati).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...