CHUO kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam wamesheherekea siku ya Mwanamke Dunia kwa Kuzungumza yapasayo mtoto wa kike na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Hananasif jijini Dar es Salaam leo.

Wanafunzi hao wameaswa kusoma masomo ambayo hayatumii watu wengi na kusoma masomo ambayo yanatumia rasilimali ili iwe rahisi kuajiliwa na kujiajili wenyewe.

Hayo ameyasema Mhadhiri mwandamizi wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dkt. Godbertha Kinyondo jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo kilele chake ni Machi 8,2020. Amesema kuwa sekta ambazo ni nzuri kwa mtoto wa kika ni sekta ambazo hazitumii watu wengi na zinazotumia rasilimali tuu.

Hata hivyo Godbertha amewabainishia sekta zinazikuwa kwa kasi zaidi kuwa ujenzi, fedha, mawasiliano, madini na utawala wa umma na kuwataka waingie kwani ni sekta zinazokuza uchumi zaidi.

"Mimi nataka nyie mjitayarishe muingizwe katika sekta za ujenzi, fedha, mawasiliano, madini na utawala wa umma  kwa sababu ndizo zinakuza uchumi zaidi na ndizo zenye hela zaidi." Amesema Dkt  Godbertha

Hata hivyo mwaka 2020 ni mhimu kwa wanawake wote hasa wa Afrika kwa kutimiza miaka 25 tangu Getrude Mongella kuongoza mkutano wa kimataifa wa wanawake huko Beijin nchini uliokuwa kwaajili ya kutetea haki za mwanamke na kauli mbiu ya mwaka huu kwa Tanzania katika kuadhimisha siku ya Mwanamke duniani ni "Kizazi sawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae."

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni (UNESCO) zinasema kuwa Tanzania elimu imeimarika kwa watoto wa kike imefikia asilimia 95.39 ambayo inazidi watoto wa kiume kwa elimu ya awali, msingi na Sekondari.

Kwa upande wa Afya Godberther  amesema kuwa  nguvu kazi ambayo ni mwanamke kwa Takwimu za  HTDHS za 2015-2016 zinaonyesha kuwa wanawake 556 kati ya vizazi 100,000 wanapoteza maisha wakati wanajifungua  huku mwanamke ingawa mafanikio makubwa yanaonekana katika sekta ya afya ya kujenga zahanati na vituo vya afya ili kuhudumia jinsia zote.

Hata hivyo amewaasa wanafunzi wa mashuleni kupewa elimu za uongozi katika taratibu zote za uchaguzi na kuwepo na miongozi na sheria zinazoelekeza mtoto wa kike na wakiume kugombea nafasi za uongozi.

Godbertha amesema kuwa jamii lazima itambue na kuheshimu haki za binadamu hasa za wanawake na walemavu, katika kubeba ajenda yenye ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.

Licha ya hivyo Godbertha amekemea unyanyasaji na udhalilishaji wa mwanamke na watu wenye ulemavu katika jamii.

Kuhusu rushwa ya ngono amesema imekuwa ikipoteza malengo kwani Mwanamke anavyotoa rushwa ya ngona inampotezea ujasiri wa kusimama na kujitetea kulingana na nafasi alipo.

Hata hivyo vyombo vya habari hapa nchini vimeaswa kutangaza zaidi nafasi ya mwanamke katika jamii, haki za mwanamke pia kuepuka kutumia lugha zinazodhalilisha utu wa mwanamke na kutumia jumbe za utetezi wa mwanamke.

Kwa upande wake Mwanasheria na Mjasiliamali ambaye alishinda tunzo mwaka jana, Vincesia Fuko amewaasha wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Hananasif kutokukaa kimya endapo jambo linalowapotezea malengo yao ya kimasomo lonapotokea na kutoa taarifa katika madawati ya jinsia au katika serikali za mtaa zilizopo karibu.

Wanafunzi  kutoka shule ya Hananasif waliozungumza na wahadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe ni wananfunzi wasichana wa kidato cha pili, kidato cha tatu pamoja na kidato cha nne.
Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Godbertha Kinyondo akizungumza na wasichana wa shule ya Sekondari ya Hananasif jijini Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha siku ya Mwanamke duniani ambapo hitimisho la siku ya mwanamke ni Machi 8 ambayo hufanyika kila mwaka. Amewashauri kusoma masomo amayo hayatumia rasilimali watu na kuchukua masomo yanayo tumia rasilimali ili kuendana na mapinduzi ya Viwanda na teknolojia.
 Mkuu wa Idara ya kozi fupi na shauri za kitaalam ambaye alimwakilisha  mkuu wa chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam, Faisal Issa akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Hananasif  jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya wanawake dunia ambapo kwa mwaka huu kuwa mhimu kwa kutimiza miaka 25 tangu mkutano wa Beijin China kufanyika kwa kutetea haki za mwanamke. kushoto ni Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Godbertha na kulia ni Mwanasheria na mjasiliamali, Vincesia Fuko.

 Wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Hananasif jijini Dar es Salaam wakisikiliza mtoa maada.
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Yusuf Zuberi akichangia maada wakati wa chuo cha Mzumbe wakisheherekea siku ya wananwake kwa kuwapasomo wanafunzi wasichana wa shule ya Sekondari ya Hananasif ya jijini Dar es Salaam.
 

 Mwanasheria na mjasiliamali, Vincesia Fuko akizungumza na wanafunzi wasichana wa shule ya Sekondari ya Hananasif jijini Dar es Salaam, huku akiwaasa wasikae kimya ambapo vitendo vi aya vikiwakuta na kutaka kukatisha ndoto zao katika kujipatia elimu hapa nchini. Hii ikiwa ni kuadhimisha siku ya Mwanamke duniani.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Hananasif wakiuliza maswali leo katika kusheherekea siku ya mwanamke amayo hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8. 








Picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...