Na Zainab Nyamka, Michuzi Glob.
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na Pwani DAWASA wametekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa asilimia 100.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya Dawasa iliyopo Mkoa wa Pwani.

Ndikilo ameanza ziara ya siku mbili kutembelea miradi hiyo, ambapo ameipongeza Dawasa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusambaza maji kwenye maeneo muhimu ikiwemo Kiwanda cha Nyama Tan Choice kilichopo Kibaha wenye thamani ya Bilioni 1.1 , Mradi wa maji la Chalinze Mboga na eneo la Viwanda ambapo kufikia mwezi Julai unatarajia kuanza.

Akizungumza baada ya kumaliza ziara yake kwenye chanzo cha maji Wami, Ndikilo amesema Miradi mingi inayofanywa na Dawasa ni maelekezo ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na wametekeleza kwa asilimia kubwa sana.

Amesema, ndani ya Mkoa wa Pwani kuna miradi mingi inaendelea kujengwa na Dawasa na ziara hii itasaidia kuboresha maeneo ambayo hajayafanya vizuri.

" Naipongeza Dawasa, imefanya kazi kubwa sana kutuletea maji katika Mkoa wa Pwani, na hii wametekeleza agizo la Rais alipotembelea mkoa wa Pwani 2016," amesema.

"Vyanzo vikuu vya maji vipo katika Mkoa wetu wa Pwani, Ruvu Juu na Ruvu Chini haiwezekani maji yaende Dar es Salaam halafu hapa kwetu hakuna nafurahi sasa miradi ya maji ipo mikubwa," 

Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja  amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Pwani kupata maji ya uhakika ambapo sasa hivi wanaendelea kutekeleza miradi iliyopo na itakapokamilika maji yapatikana muda wote.

Amesema, wamepeleka maji katika Kiwanda cha nyama wakitumia fedha za ndani bilioni 1.1 wakichukua maji kutoka bomba kuu linalotokea Mlandizi litakalopeleka maji Lita Milion 2 kwa siku.

Naye Mbunge wa Jimbo la Chalinze Riwadhan Kikwete ameishukuru serikali ya awamu ya tani chini ya Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha mkoa wa Pwani unapata maji ya uhakika.

Katika ziara hiyo, Wananchi wameaswa kulinda vyanz vya maji na kuacha kufanya shughuli za kijamii mita 60 kutoka kwenye mto pamoja na kulipa bili za maji ili Dawasa iweze kujiendesha na kujenga miradi mingine mipya.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja baada ya kutembelea eneo lililounganishwa bomba kuelekea katika Kiwanda cha Nyama Kibaha (Tan Choice) wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA Mkoani Pwani
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo mafupi ya miradi kwa  Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Mhandisi Evarist Ndikilo kabla ya kuanza kutembelea miradi inayoendeshwa na Dawasa.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Mhandisi Evarist Ndikilo akipokea maelezo ya uzalishaji wa kiwanda cha kisasa cha Nyama kibaha (TANCHOICE) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  Rashid Abdulah(wa kwanza kushoto)  wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA Mkoani Pwani.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Katibu Tawala wa Mkoa wa pwani Bi Theresia Mbando wakati wa kutembelea miradi ya Maji Mkoa wa Pwani.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kulia) akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa chanzo cha maji cha Wami wakati wa kutembelea mirafi ya Maji Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kulia) akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa chanzo cha maji cha Wami wakati wa kutembelea mirafi ya Maji Mkoa wa Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...