Na Woinde Shizza ,KARATU
Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Muhongo amewapongeza watendaji wa Halmashauri kwa kuandaa bajeti bora iliyokidhi mahitaji ya kila sekta.
Aliyasema hayo juzi katika Kikao maalumu cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, na kuongozwa na mkuu wa wilaya hiyo ambaye pia ni mwenyekiti katika Kikao hicho ambacho jukumu lake ni kushauri na kilifanya mapitio ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kuridhia kupitisha bajeti hiyo.
Alisema kuwa upangaji wa bajeti mwaka huu umeongezeka kwa kiasi ambapo aliwapongeza watendaji wa Halmashauri kwa kuandaa bajeti bora iliyokidhi mahitaji ya kila sektaubwa
Makadirio ya bajeti ya fedha mwaka ujao ni takribani shilingi billion 3.9 tofauti na makadirio ya sasa ambayo ni shilingi billion 3.3.ambapo aliwapongeza Halmashauri kwa kufika kiwango cha 50% ya ukusanyaji wa mapato kwa robo iliyomalizika ya mwaka huu wa fedha na kubainisha kuwa hi ni ishara njema na kuongeza kuwa fedha za mapato ndizo zinatolewa na serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mahongo alisema anataka mapato ya mwakani yafike kiwango cha billion 4, na kufafanua kuwa Karatu kuna vyanzo vingi sana vya mapato lakini bado hatuvitumii vizuri huku akitolea mfano mathalani ziwa Eyasi watu wanavua samaki kinyemela na kusafirisha lakini hakuna mapato yanayopatikana, Alimpa Malekezo Afisa mifugo kwenda kushughulikia changamoto hiyo mapema iwezekanavyo kabla hajachukua hatua kali zaidi.

"kikosi kazi kimeshawahi kukamata ndoo 20 ,pia wamekamata ndoo77 za samaki ambazo hazijalipiwa ushuru ,hawezi kuvumilia upotevu huo wa mapato katika eneo langu nielekeze mashine za malipo kwa njia ya mtandao POS zipelekwe Mang’ola na Afisa tarafa pamoja na Afisa mifugo washirikiane kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali, Njia zote zinazoaminika samaki wanapitishwa wawekwe watu ili kuhakikisha stakabali zinatolewa na watu wanakuwa huru kuendelea na shughuli zao za uvuvi wa samaki "alifafanua Mahongo
Aidha alimuelekeza Afisa mifugo kuhakikisha hakuna uvuvi haramu unaofanyika kwa kutumia kokoro ,Uvuvi ambao unaharibu mazalia ya samaki wadogo, huku akiwataka kujipanga na kutoa taarifa za utekelezaji wa maelekezo yake ,Lakini pia aliwasihi wawape uhuru wananchi kuendelea kujihusisha na shughuli za uvuvi kwa sababu ziwa limejaa maji na lina samaki wengi kwa sasa.
Mahongo ameonesha kusikitishwa na utoro wa wanafunzi katika kata ya Kansay baada ya kupokea taarifa ya watoto 80 ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza katika na shule ya sekondari Kansay ,Alimuelekeza mtendaji wa kata ya Kansay kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha watoto hao wamejiunga na elimu ya sekondari, huku alibainisha kuwa shule ya Kansay ina madarasa ya kutosha baada ya kukamilika jengo la utawala, awali walimu walikuwa wanatumia vyumba viwili vya madarasa kama ofisi ambavyo sasa wanafunzi wanavitumia.
Alimalizia kwa kuwaasa wananchi kutocheza na elimu, huku akiwataka watendaji wachukue hatua kali kwa wazazi walioshindwa kupeleka watoto shule, ameomba viongozi wa dini kumsaidia kutoa elimu ya ufahamu kwa wananchi juu ya umuhimu wa elimu.
Alisema maendeleo hayana lelemama, kwa sasa hatuwezi kueleweka ila baadae ndio tutaeleweka tunachosisitiza ,Bila ya elimu tumekwisha tukipata elimu maradhi yatakwisha, umasikini utakwisha, tukicheza nayo tutaumia.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Muhongo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...