Waandaaji wa Kongamano la Shinyanga Women's Day Out wakiwa ukumbini.
Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.
Meza Kuu 'VIP' wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.
Mwenyekiti wa maandalizi wa Kongamano hilo Fausta Kivambe, akitoa shukrani kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out
Kongamano la wanawake Shinyanga mjini (Women's Day Out), lililoandaliwa na Kikundi cha Wanawake na mabadiliko (Women for Change - WFC ), limehudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka Shinyanga mjini, kwa ajili ya kupewa elimu mbalimbali ikiwamo ya malezi, afya, sheria, pamoja na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.
Kongamano hilo limefanyika leo Machi 7, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, Mboneko aliwataka wanawake Shinyanga mjini washirikiane na kuungana mkono, ikiwamo kwenye masuala ya kuinuana kiuchumi na kuacha tabia ya kutopendana.
Alisema huu ni wakati wa wanawake kushirikiana, kupendana na kuungana mkono kwenye masuala ya kibiashara kwa kununuliana bidhaa, na kuacha tabia kutopendana ili wapate kusonga mbele kiuchumi.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kutumia vyombo vya habari na mitandao ya jamii kutangaza shughuli wanazofanya.
“Napongeza sana kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko cha Women for Change kwa kufanya Kongamano hili la wanawake Shinyanga mjini, na hasa kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni Machi 8,2020 kwa kukutanisha wanawake kupewa elimu mbalimbali kwa mstakabali wa maisha yao,”alisema Mboneko.
“Kupitia Kongamano hili naomba wanawake, mpendane, mshirikiane, pamoja na kuungana mkono kwenye biashara mbalimbali ili mjikwamue kiuchumi, ambapo dhana za kuchukiana zilishapitwa na wakati, kipindi hiki ni cha mabadiliko wanawake tuungane na kuwa kitu kimoja,”aliongeza.
"Pia nakipongeza kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko kwa kufanya ukarabati wa bweni la wavulana kwenye kituo cha kulea watoto wenye ualbino Buhangija, ili kuwaweka katika mazingira mazuri, mfano ambao unapaswa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo",alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha wanawake na mabadiliko 'Women for Change, kutoka Shinyanga mjini Getrude Munuo, alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2013 na 2014 walipata usajili, na lengo lao kubwa ni kusaidiana kuinuana kiuchumi pamoja na kufanya shughuli za kijamii.
Alisema wameendesha kongamano hilo kwa lengo la kutoa elimu mbalimbali kwa wanawake wa Shinyanga mjini, ikiwamo ya malezi, afya pamoja na namna ya kushirikiana kibiashara ili kuinuka kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...