Na Amiri Kilagalila, Njombe

Mkuu wa wilaya ya Njombe mkoani humo Ruth Msafiri amesema  haiwezi kupita siku moja mkoani Njombe bila kupata matukio ya ukatili yanayojumuisha ukatili wa kingono yasiyopungua 6-12  hali inayoweza kusababisha mkoa huo kuwa na matukio mengi ya ukatili kwa mwaka.

Ruth Msafiri ameyasema hayo mjini Makambako mkoani Njombe wakati wa msafara wa kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia unaopita karibu mikoa yote nchini  kutoa elimu kwa wananchi kwa lengo la kuleta usawa wa kijinsia kwa maendeleo ya taifa kuelekea siku ya wanawake duniani itakayofanyika machi nane mwaka huu.

“Masimango,masengenyo,kunyima amani lakini pia ukatili wa kingono,haiwezi kupita siku moja Njombe bila kupata matukio kimkoa yanayoanzia sita mpaka kumi na mbili,kwanza kuna ubakaji wa hali ya juu sana peke yangu katika wilaya  yangu kwa wiki napokea matukio yasiyopungua manne”alisema Msafiri

Joseph Magazi ni afisa mradi wa shirika la msaada wa kisheria na Melda Kamugisha ni afisa mkuu wa maendeleo ya jamii wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto wanasema asilimia 9 ya wanawake wa umri kati ya  miaka 15 hadi 49  wameingiliwa kimwili nchini.

“Asilimia 40 ya wananawake wenye umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja au zaidi katika kipindi cha maisha yao,kadhalika asilimia 9 ya wanawake wa umri kati ya miaka 15-49 wameingiliwa kimwili bila ridhaa yao”alisema Melda Kamugisha ni afisa mkuu wa maendeleo ya jamii wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.

Mkoani Njombe msafara huo umezulu mjini Makambako ambapo baadhi ya wakazi wa mji huo akiwemo elizabeth mlunga wametaka ndugu wa mume wawe wanatambua haki za mke pindi anapofiwa na mumewe.

Vile vile kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,mkuu wa wilaya  ya Njombe Ruth Msafiri amesema baadhi ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia mkoani hapo yanasababishwa na mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...