LEO Machi nane dunia inaadhimisha ya siku mwanamke duniani na hapa nchini mashirika na taasisi mbalimbali zimeadhimisha siku hiyo kwa namna mbalimbali huku kauli mbiu ikiwa ni "Kizazi Cha usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na baadaye." na kwaupande wa Ecobank Tanzania wameadhimisha na kusherekea kwa kujizatiti zaidi katika kuhakikisha wanawake kutoka Benki hiyo pamoja na wote wanaozunguka jamii wanainuliwa katika nafasi mbalimbali.

Maadhimisho hayo yaliyofanywa na Ecobank leo jijini Dar es Salaam ya yamebeba dhamira kubwa kwa Benki hiyo hasa kwa kuendelea na kuzingatia uwakilishi wa mwanamke mahala pa kazi huku ikielezwa kuwa nafasi ya mwanamke katika uongozi ni faafu na yenye tija hasa kwa kuleta matokeo chanya.

Imeelezwa kuwa wakiwa Benki ya Panafrican wataendeleza juhudi zaidi katika kuwainua wanawake kutoka  Benki hiyo pamoja na wanawake wote wanaozunguka jamii ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu.

Maadhimisho hayo yalienda sambamba na kupata kifungua kinywa na kukata keki kwa pamoja kama ishara uimara wa mwanamke katika ushiriki wa nafasi mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo wakati wa maadhimisho ya sku ya wanawake duniani inayoazimishwa tarehe 08 kila mwaka ikiwa na kauli mbiu ya Uwajibikaji wa Uongozi katika kujenga Kizazi cha Usawa wa Jinsia.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...